Kwanza
nianze kwa kuwatakia Waislamu wenzangu wote Mfungo mwema wa mwezi wa
Ramadhani na Kheri za mfungo huu zimulike katika nyumba zote, nchi zote
na wale wote ambao kwa namna moja au nyengine wameshindwa kufunga mwezi
huu kwa sababu mbalimbali ikiwemo hali duni ya maisha, maradhi au
kubanwa na hali ambazo zinawalazimu wasipate thawabu za funga.Ni imani
Mungu mwenyezi atawaangazia na kufanya wepesi kuwaondoa katika hali
hiyo.
Niwaombee salaam Wadogo zangu
waliotekwa Nigeria, na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kama
vita.Kwangu ni dua kipindi hiki ili kuweka wepesi katika kuwatoa katika
dhiki hizo kubwa.
Pia nitumie nafasi hii kuuambia
Umma wa Tanzania na hasa wale watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao
wameendelea kuwa waathirika wa matumizi mabaya ya mitandao kuwa Hii
ndiyo Account rasmi ya Ridhiwani Kikwete. Hizo account zingine ikiwemo
Ridhiwani J. Kikwete
Ridhiwani Kikwete official fan page
Ridhiwani Kikwete birth date 1983
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Ridhiwani Kikwete -nimevaa shati la Ccm
Na nyenginezo si account zangu,ni
za watu ambao wamejisikia kutumia jina langu kwa sababu mbalimbali jambo
ambalo nimeona katika siku hii ya leo nilikanushe. Kwa kauli ya
kukanisha namaanisha kuwa hizi account sina mahusiano nazo kabisa na
hawa wanaotumia Jina langu nawaomba waache mara moja kwani si jambo jema
kuoongopea ummma wa Watanzania ambao wamekaa mitandaoni wakiamini
wanafanya mawasiliano nami wakati kihalisia si mimi.
Mwisho, napenda kuwaambia Watanzania na wana mtandao wenangu kuwa haya Makundi yaliyoanzishwa kwenye mtandao kama
-YOUTH BATTLE
-VIJANA WANAOIPENDA NCHI YAO KWA MOYO
-SACCOS INAYOTOA MIKOPO
-UNGANISHAJI BODI YA MIKOPO etc.
Na mengineyo ni makundi ambayo
sijawahi na wala sijashiriki kuyaasisi mimi.Ni hao ambao hawana nia
njema na jina langu na heshima ya familia ambayo nimekuwa nahangaika
kuihifadhi.
Account yangu halisi ni
RIDHIWANI KIKWETE ambayo
kwenye profile picha yangu yuko bwana Reginald Mengi na Juzi nilitoa
tangazo kukanusha habari za msiba wa Ndg.Shukuru Jumanne Kawambwa(Mb) wa
Bagamoyo.
Hivyo naomba kutoa angalia kwa Watanzania wenzangu.
Nawaomba kuwasilisha.
Mimi
RIDHIWANI KIKWETE
Post a Comment