Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANGAZO LA NECTA KWA WATAHINIWA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2015

 
 
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi,Mei 2015 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilianza rasmi tarehe 1 Julai, 2014 hadi tarehe 30 Septemba, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=.   Aidha kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2014 hadi tarehe 31 Oktoba, 2014 waombaji watajisajili kwa ada ya Shilingi 65,000/- (ada pamoja na faini).
 
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya  mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mtihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-pesa.
 
Imetolewa Na:
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Mitihani la Tanzania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top