Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania.
Kaimu
Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James
Andilile (kushoto) akijibu maswali toka kwa waandishi wa habari
waliohudhuria Mkutano uliohusu Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa
kuchimba mafuta nchini Tanzania baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa
baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari zilizokinzana kuhusu Kampuni
hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) Bw. Yona Killagane.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria Mkutano huo wakifuatilia kwa
makini taarifa ya ufafanuzi iliyokuwa ikitolewa na baadhi ya Viongozi wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu Kampuni ya
Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Na Benedict Liwenga na Winner Abraham-MAELEZO.
SHIRIKA
la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC limetoa ufafanuzi kuhusiana na
Kampuni ya Statoil yenye mkataba wa kuchimba mafuta nchini Tanzania
baada ya kutokea kwa mkanganyiko kwa baadhi ya vyombo vya habari
kuandika habari zilizokinzana kuhusu Kampuni hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. Yona
Killagane ameeleza taarifa zilizo sahihi kuhusu kampuni ya Statoil na
mikataba yake mbalimbali na Serikali katika upataji wa faida kutokana
na utafutaji wa mafuta na gesi .
Killagane
ameeleza kuwa utaratibu unaotumika katika kutafuta mafuta ni aghali
sana na ni hatari kwa maisha, hivyo serikali haiwezi yenyewe kuingia
gharama hizo za utafutaji na badala yake inatumia mifumo mbalimbali kama
vile Concession agreement, Service agreement pamoja na Mkataba wa kugawana mapato ambapo
kati ya mikataba hiyo mitatu Serikali inatumia mkataba wa kugawana
mapato ambapo humpa mwekezaji kazi kisha rasilimali zikigunduliwa
hugawana na kampuni hiyo au mwekezaji aliyegundua. Hivyo serikali
inategemea kupata mrahaba na kodi toka kwa makampuni inayoingianayo
mikataba.
Kwa
upande mwingine Mkurugenzi amevieleza vyombo vya habari kuwa ugunduzi
wa gesi unategemea miundo mbinu mingi sana na inategemea uwingi wa gesi
hiyo ndiyo maana serikali inaingia mikataba na makampuni makubwa yenye
uwezo mkubwa wa kifedha ili kuweza kufanya utafiti na kuchimba mafuta na
gesi.
Aidha,
Bw. Killigane amefafanua kuwa mkataba walioingia kati ya Serikali na
kampuni ya Statoil mwaka 2007 ulikuwa ni wa kutafuta mafuta na sio gesi
lakini hapo mwaka 2012 mkataba mwingine wa kutafuta gesi ulifanyika kati
ya kampuni hiyo na Serikali.
“Statoil
ilipendekeza kuwa kwenye mgao wa mkataba wa mwanzo serikali ipate
asilimia 5% statoil asilimia 95% kama zabuni iliyokuwa imeletwa, lakini
baadaye kamati ikakaa na kuzungumza na mwekezaji ambapo mwekezaji
aliweza kusukumwa kutoka asilimia 5% hadi asilimia 30% na hivyo hii
ilijumuisha TPDC kuweza kujiunga kwa asilimia 10%, kwa sasa katika
mkataba wa mafuta serikali inapata asilimia 56% na Statoil asilimia 44%,
katika mkataba wa wagesi serikali inapata asilimia 61% na mwekezaji
asilimia 39% katika kipindi cha mkataba”. Alisema Killigane.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw.
James Andilile aliwahakikisha waandishi wa habari kuwa serikali iko
tayari kusaidiana na waandishi wa habari katika kutoa taarifa sahihi ili
kuweza kuwaeleza watanzania kuhusiana na sekta ya mafuta na gesi na
nini kinaendelea.
“Hii
nchi ni yetu na kazi zote tunazozifanya ni kwajili ya watanzania, jinsi
waandishi wa habari wanavyotoa taaarifa zisizo sahihi wanaharibu sura
ya nchi yetu na kuwapa hofu wawekezaji na hivyo kuleta hasara badala ya
faida, kama kuna jambo lisiloeleweka tunawaomba kwa wakati wowote
mkituita tutakuwa tayari kuwapa taarifa ili wote kuwa katika ufahamu
mmoja”. Alisema Andilile
Post a Comment