Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UWOYA BANA ! AFANYA FUJO KUBWA YA KUFA MTU NYUMBANI KWA MUME WA MTU



NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras
Uwoya amesababisha tena ! Safari hii amekinukisha
nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi
wake ( jina tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga
ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya
kuendelea kuwa ‘ nyumba ndogo ’ .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua
nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo,
Sinza- Mori jijini Dar es Salaam.
Nyota wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya
MCHEZO ULIVYOKUWA
Chanzo kilidai kwamba , siku ya tukio , Uwoya akiwa
na baadhi ya mastaa wenzake ( hawakutajwa)
kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu
mjini Bagamoyo , Pwani, alipokea simu
iliyomnyetishia kuwa , mpenzi wake huyo amefunga
ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza , kwa
hiyo yeye aliye tu !
UWOYA ACHANGANYIKIWA
“Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu
alichanganyikiwa ! Alianza kusema maneno ya
kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio . Mbaya
zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo
ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi .
“Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake
na kwamba atamtambua kwani nia yake ilikuwa
kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo na huyo
mke mpya , ” kilisema chanzo hicho cha uhakika .
Nyumba anayodaiwa kufanya fujo
AANZIA DUKANI
Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii
wenzake kumsihi asichukue hatua hiyo anaweza
kuishia polisi , Uwoya hakukubali, aliondoka kwa
hasira na breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye
duka kubwa la jamaa huyo lililopo Mikocheni , Dar
ambapo alifanya fujo.
“Kule alipogundua huyo mwanaume wake hayupo
ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza
ambako aliendeleza fujo zake kwa kutukana na
kutishia mambo mengi, ” chanzo kilisema .
HASIRA PEMBENI
Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri kuwa , Uwoya
aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘ kujaza
nzi ’ ( watu kuwa wengi ) ambapo aliondoka
mdogomdogo na kama hana hasira utadhani si yeye
aliyekuwa akichafua hali ya hewa .
MATEGEMEO YAKE
Habari za ndani ziliendelea kudai kuwa , Irene
alishikwa na hasira za jamaa huyo kuoa kwa vile
alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya
ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda,
Hamad Ndikumana ‘ Katauti’ kwenda halijojo!
“Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia
jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri,
ilimfanya aishiwe nguvu ,” kilisema chanzo.
ALICHOAMINI
Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni
kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa
kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘ nyumba ndogo ’
jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo .
UWOYA HUYU HAPA
Baada ya gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima,
lilimsaka staa huyo na kubahatika kukutana naye
maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba,
alishaachana na mwanaume huyo.
“Ilitokea, lakini nilishaachana naye . Unajua ishu si
kwamba angenioa mimi , ila kitendo alichokifanya
hakikuwa cha uungwana , ” alisema Uwoya .
AMWANGA CHOZI
Katika hali isiyotarajiwa , msanii huyo alianza
kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale
alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka
tukio la jamaa yake kufunga ndoa kwa siri au la!
Uwoya: “We niache tu , nina mambo mengi sana
yanayoniliza mimi .”
Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana
kwa njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa
kifupi: “Haiwahusu .” Kisha akakata simu.
HISTORIA
Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa Julai 11, 2009
kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la
Dar es Salaam. Mei 8, 2011 walijaliwa kupata mtoto
wa kiume aitwaye Krish .
Hata hivyo , Novemba 16, 2011 kwenye gazeti hili
kuliandikwa habari yenye kichwa;
NDOA YA UWOYA YAVUNJIKA.
Ndoa hiyo iliparaganyika baada ya Uwoya kudaiwa
kumkataa mwanaume huyo na mpaka sasa
haijasimama tena huku mwanaume akiwa kwao ,
Rwanda.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top