Shinji
Kagawa (kushoto), Darren Fletcher (katikati) na Tom Cleverley (kulia),
wakishangilia baada ya kuifunga Inter Milan kwa penalti 5 -3.
Fletcher na David De Gea wakishangilia kwa pamoja.
Fletcher akimkumbatia, Michael Kean (kushoto) baada ya ushindi.
KOCHA Louis
van Gaal ameendeleza wimbi la ushindi baada ya Manchester United
kuifunga Inter Milan kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 0-0 katika mchezo
wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika
mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington,
penalti za United zilitiwa nyavuni na Ashley Young, Javier Hernandez,
Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli
wa Inter aligongesha mwamba. Van Gaal akipanga vikosi viwili, kimoja
kila kipindi.
Man United kipindi cha kwanza: Lindegaard, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney, Welbeck
Kipindi cha pili: De Gea; M Keane, Evans, Blackett; Young, Cleverley, Fletcher, Kagawa, Shaw; Zaha, Nani/Hernandez dk77.
Inter Milan: Handanovic/Carrizo
dk63, Ranocchia, Vidic/Andreolli dk72, Juan Jesus, D'Ambrosio,
Jonathan, Kuzmanovic/Laxalt dk63, Krhin/M'Vila dk46, Dodo/Nagatomo dk63,
Botta/Taider dk63 na Icardi.
Post a Comment