Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe (kulia) na Naibu Mkurugenzi wake Hamad
Koshuma (kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa polisi walipofikishwa
Mahakama ya Hakimi Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaa jana kujibu mashtaka
ya matumizi mabaya ya madaraka.
*********
Mgawe mshtakiwa mwingine, Naibu Mkurugenzi Mkuu PTA, Hamadi Koshuma jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Isaya Arufani.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Osward Tibabyekomya akisaidiana na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Ben Linkolin ulidai kuwa Desemba 5, mwaka 2011 katika ofisi za TPA, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa mamlaka hiyo kwa nyadhifa hizo, walitumia vibaya madaraka yao.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa walitumia vibaya madaraka yao baada ya kusaini mkataba kati ya TPA na Kampuni ya China Communications na kuipa kazi ya ujenzi wa gati namba 13 na 14 la mamlaka hyo bila kutangaza zabuni kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria ya manunuzi namba 21 ya mwaka 2004.
Washtakiwa walikana mashitaka hayo na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hauna pingamizi la dhamana.
Hakimu Arufani alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana ikiwa watatimiza masharti ya kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh.
milioni mbili na wadhamini wawili wanaofanyakazi taasisi za kuaminika watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani hiyo ya fedha.Washtakiwa walitimiza masharti hayo na wako nje kwa dhamana hadi Agosti 13, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.
Awali, katika viunga vya mahakama hiyo walifurika watu wanaodaiwa kuwa wanafamilia wa washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao.
Agosti 23, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe, alimsimamisha kazi Mgawe na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kufanyika.
Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kwa tuhuma za kupoteamafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment