Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ wakikata mauno.
Hatimaye! Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa na kusababisha tafrani kubwa, Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ hatimaye wamekutana uso kwa uso (live) na kumaliza bifu lao saa chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,
NI KWENYE VUNJA JUNGU
Tukio
hilo la heshima lilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa staa mwenzao wa
sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, Mwananyamala jijini Dar ambapo
baadhi ya mastaa walikuwa wakivunja jungu katika sherehe ya kumpongeza
rafiki yao almaarufu kwa jina la Wise Ime aliyejifungua mtoto wa kike
hivi karibuni.
KWA MARA YA KWANZA TANGU WAGOMBANE
Katika tukio hilo, mastaa wenzao walipigwa na butwaa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu wagombane. miezi kadhaa iliyopita.

WALA UJANA KAMA ZAMANI
Mastaa hao walinaswa pamoja wakiwa kama kumbikumbi wakila ujana kama zamani, kitendo kilichowafurahisha marafiki zao wengine waliofika nyumbani hapo wakimpongeza Aunt kwa kuwaweka pamoja kwani tangu wapatanishwe hawakuwahi kukaa pamoja wala kula sahani moja kama walivyofanya siku hiyo.

“Ukweli
sisi tumefurahishwa na ukaribu wa hawa mashosti tuliwamisi sana kuwaona
hasa kwenye shughuli kama hizi za kibao kata, leo wameshirikiana kama
zamani, wamezungumza, wamecheka na kukata mauno pamoja,” alisikika mmoja
wa mastaa aliyehudhuria katika shughuli hiyo.
MAUNO MWANZO-MWISHO
Kwenye shughuli hiyo kulipambwa na mauno mwanzo-mwisho yaliyoongozwa na wapiga ngoma ya Kibao Kata ambapo kila mmoja aliinuka na kuonesha ustadi wake wa kukata mauno.

HADI MAJOGOO
Shughuli hiyo iliendelea hadi majogoo kwani baada ya Kibao Kata, mastaa hao walifunguliwa disko lililokuwa likiongozwa na madj maalum wa Pro24djs huku MC akiwa ni Maimartha Jesse.

WEMA, KAJALA, AUNT WAPAGAWISHA
Katika shughuli hiyo, Wema, Kajala na Aunt walipagawishwa na wimbo wa mpya wa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wa Mdogomdogo ambapo waliingia kati na kuachia mauno hadharani.

Kuna
wakati Kajala na Wema waliachiwa nafasi ambapo walitoana jasho kwa
kukata mauno huku wakifuatisha vizuri wimbo huo utadhani walikuwa
wamefanya ‘riheso’.
ASANTE DJ
Baada ya kuserebuka kwa muda mrefu hadi wakatoka jasho, wawili hao walisikika wakisema kuwa Dj alikuwa amewakuna mno kwani kila muziki aliokuwa akiwawekea alikuwa akiwalenga na kuwafanya wachangamke zaidi hadi shughuli ilipokwisha kila mtu akarudi kwake.

NENO LA WEMA
“Sasa hivi tupo vizuri sana. Yes tupo bega kwa bega ukizingatia ndiyo tunaingia kwenye mwezi mtukufu. Nimefurahi sana kushea naiti na Kajala,” alisema Wema.

NAYE KAJALA
“Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo. Sisi tupo vizuri kama alivyosema Wema tumeinjoi sana,” alifunguka Kajala.

TUMEFIKAJE HAPA
Miezi kadhaa Wema na Kajala waliingia kwenye gogoro kubwa na kusababisha kuibuka kwa pande mbili za Team Wema na Team Kajala zilizokuwa zinachochea ugomvi huku Kajala akitakiwa kurejesha zile Sh. Milioni 13 alizolipiwa na Wema asiende jela miaka 7.

Post a Comment