Waamuzi
wa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana
wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika
Kusini (Amajimbos) wanawasili leo (Julai 15 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Mechi
hiyo itafanyika Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam na itachezeshwa na waamuzi
hao kutoka Shelisheli. Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu.
Waamuzi
hao ambao wanawasili saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ni
Allister Barra, Gerard Pool, Jean Joseph Felix Ernest na Nelson Emile
Fred.
Kamishna
wa mechi hiyo Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar pia
anawasili leo saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
Post a Comment