Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MAGUFULI AZINDUA KIVUKO KIPYA BUNDA

DSC_1839
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEFUNGUA RASMI KIVUKO CHA MV MARA CHENYE UWEZO WA KUBEBA TANI 25 YANI MAGARI MANNE( 4) NA ABIRIA 50 KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA IRAMBA WILAYA YA BUNDA NA MAJITA WILAYA YA BUTIAMA
DSC_1815
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKITOA MAELEKEZO KWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISI MUSSA IYOMBE KUSHOTO HUKU MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA HERBERT MRANGO PAMOJA NA MTENDAJI MKUU WA TEMESA MAMA MARCELINA MAGESSA WAKISIKILIZA KWA MAKINI.


DSC_1839
PICHA YA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KAMA KINAVYOONEKANA KATIKA PICHA KABLA YA KUFUNGULIWA
DSC_1920
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPOKEA ZAWADI ZA KIMILA KUTOKA KWA WENYEJI WA BUNDA ZA KUMTAMBUA KUWA MKAZI WA MJI HUO KWA KIMILA.
DSC_1973
WAZIRI WA UJENZI MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA WAKAZI WA IRAMBA KATIKA JIMBO LA MWIBARA KABLA YA KUZINDUA KIVUKO CHA MV. MARA CHENYE UWEZO WA KUBEBA TANI 25 YANI MAGARI MANNE NA ABIRIA 50
DSC_2044
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIFURAHIA NA WANACHAMA WAPYA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WALIOAMUA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO MARA BAADA YA WAZIRI MAGUFULI KUMALIZA KUHUTUBIA MKUTANO.
DSC_2087
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA BUNDA NA MAJITA MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA MHANDISI EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MWIBARA ALPHAXAD KANGI LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISHI MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA.
DSC_2104
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIBONYEZA KITUFE CHA KIVUKO CHA MV MARA KUASHIRIA KUKIZINDUA RASMI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA NA MAJITA KATIKA WILAYA MBILI ZA BUNDA NA MUSOMA VIJIJINI
DSC_2117
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIFURAHIA JAMBO NA MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA BALOZI HERBERT MRANGO HUKU MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO ALIYESIMAMA KULIA NA MBUNGE WA MWIBARA KANGI LUGORA WA KWAANZA KUSHOTO WAKIANGALIA
DSC_2187
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPUNGIA WAKAZI WA MWIBARA MARA BAADA YA KUFUNGUA KIVUKO CHA MV MARA
DSC-1212
BAADHI YA WAKAZI WA IRAMBA KATIKA JIMBO LA MWIBARA WAKIWA WAMEPANDA JUU YA MITI ILI KUMSHUHUDIA WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA KABLA YA UZINDUZI WA KIVUKO HICHO
DSC-1213
PICHA YA BOTI AMBAYO ILIKUWA IKITUMIKA AWALI KUVUSHA WATU KATI YA MAJITA NA IRAMBA KWA GHARAMA YA SHILINGI 2000/=
……………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John P. Magufuli amewataka wakazi wa Iramba na Majita kutunza kivuko kipya cha MV Mara ili kiweze kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo hayo.
Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara.
“Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani” Alisema Waziri Magufuli
Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.
Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.
“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza rasmi kuwa nauli kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli
Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.
Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri kwani ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
Taarifa hii imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Wizara ya Ujenzi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top