Waziri
wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akipokewa
na Felic Maagi Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakati alipowasili kwenye
Banda la Shirika hilo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa
TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara
ya Kirwa jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akizungumza
na baadhi ya viongozi wa shirika la nyumba nchini NHC baada ya kuwasili
kwenye banda hilo tayari kwa kukagua shughuli zinazofaywa na shirika
hilo, Kutoka kulia ni Muungano Saguya Meneja za Jamii NHC,David Shambwe Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa NHC .(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijjuka akipata
maelezo kutoka kwa maofisa wa shirika hilo wakati alipotembele banda la
NHC Kushoto ni Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha na kutoka kulia ni Elias
Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa
Mawasiliano NHC.
Mmoja
wa watu waliotembelea banda la NHC akipata maelezo kutoka kwa maofisa
wa shirika hilo kutoka kulia ni Nalindwa Norbert, Rhobi Wambura na
Wilson Sanane.
David Shambwe Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa NHC akitoa maelezo wa Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka wakati alipotembelea banda la shirika hilo kushoto ni Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha na Kutoka kulia ni Rhobi Wambura na Wilson Sanane maofisa wa NHC.
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika bana hilo.
Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Mh. Prof. Anna Tibaijuka akzungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda hilo kushoto ni Bw. Felix Maagi Mkurugenzi wa Fedha NHC.
.......................................................................................
1.Nalipongeza
Shirika la Nyumba la Taifa kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwapatia
wananchi makazi bora. Sisi upande wa Serikali tutaendelea kuwasaidia
kisera ili waweze kutimiza wajibu wao vizuri zaidi.
2. Pamoja na ujenzi wa nyumba wanaoufanya katika maeneo mbalimbali
nchini na kwa watu wa vipato vya chini na watu wa vipato vya kati na
juu, Serikali inaupongeza mpango wa Shirika waliouanza kwa kasi wa
kujenga nyumba za gharama nafuu nchini, mpango unaoendeshwa kwa
kaulimbiu ya “nyumba yangu, maisha yangu”
3. Nyumba hizo sasa zimekamilika katika maeneo 14 ya Halmashauri za miji
ikiwemo Mkinga(Tanga), Mvomero(Morogoro), Mnyakongo-Kongwa(Dodoma),
Mkuzo (Songea), Mtanda(Lindi), Mrara(Babati), Unyankumi(Singida), Kibada
na Mwongozo (Kigamboni), Bombambili(Geita), Ilembo na Inyonga(Katavi),
Uyui(Tabora), Longido na Monduli(Arusha) na Mlole(Kigoma). Miradi
mingine ya aina hii imeanza kutekelezwa katika Halmashauri mbalimbali za
Miji na Wilaya hapa nchini, lengo likiwa ni kufikia Mikoa yote na
ikibidi kila Halmashauri nchini.
4. Ili kuufanya mpango huu mzuri wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu
kuwa endelevu, mambo kadhaa ni lazima yafanyike:-
Kwanza ni kwa Halmashauri kote nchini kuunga mkono kwa kulipatia Shirika
maeneo ya kujenga nyumba hizo yasiyokuwa na masharti magumu. Ardhi
isifanywe kitegauchumi na Halmashauri kwa kuiuza kwa gharama kubwa kwani
kufanya hivyo kutafanya nyumba zinazojengwa kuwa aghali.
Pili, Halmashauri na wananchi kwa ujumla wajitokeze kwa wingi kununua
nyumba zinazojengwa na NHC ili mapato yatakayopatikana yawezeshe kujenga
nyumba zingine kwa ajili ya wananchi.
5 Zipo pia nyumba zinazojengwa katika miji mikubwa “satellite cities”
zenye lengo la kuwapatia wananchi makazi na kuondoa msongamano wa magari
mijini. Miji hiyo ni pamoja na Burka, Usar River na Mateves Arusha,
Luguruni, Kunduchi Rifle Range, Uvumba na Kawe - Dar es salaam. Aidha,
katika mikoa kadhaa hivi sasa majengo makubwa ya biashara yanajengwa ili
kuipa sura mpya miji yetu na kukuza shughuli za kibiashara.
6. Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa
hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu.
Hivyo, nalihimiza Shirika hili liendelee na mipango yake kabambe ya
kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki
nyumba. Wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa
kupunguza umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao
kupata mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
7. Nawasihi watanzania watembelee banda hili la NHC ili wapate taarifa
za kina za namna ya kununua nyumba na mahali nyumba hizo zilipo.
Post a Comment