MWIGIZAJI wa kike wa filamu Aisha Bui, amedai kuwa
alijitoa maisha yake kutoka na filamu yake ya Mshale wa Kifo, kutokana na
sinema hiyo kutengeneza porini katika msitu hatari wenye wanyama wakali.
Msanii huyo amedai alifanya hivyo kufuatia maoni ya
wapenzi wa filamu ambao kila siku wanalalamika kwa kusema kuwa filamu zetu
nyingi zimekuwa za mijini tu, huku baadhi ya matukio yakirudiwa kila katika
sinema hizo jambo ambalo limekuwa likiongelewa mara kwa mara.
“Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza
filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, lakini najua na deni kwa wapenzi
wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila
mwaka,”anasema Asha .
Filamu ya Mshale wa Kifo Imetengenezwa na Yuneda
Entertainment na imewashirikisha wasanii nyota kama Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’,
Asha Bui, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ na wasanii wengine.
Sinema hiyo imerekodiwa Mkoani Morogoro Vijijini ikiwa
ni hatua nyingine kwa watayarishaji wa filamu kwenda kucheza filamu nje ya jiji
la Dar es Salaam kama ilivyozoeleka, Aisha anasema kuwa maeneo yanayotumika
yanarudiwa sana hata baadhi ya watazamaji wameyashika kwani yanaonekana kila
filamu.
Post a Comment