Wema Isaac Sepetu akiwa kwenye pozi naNasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
Na Shakoor Jongo
Kutoka
moyoni? Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa
amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina cha
kukuhabarisha.
Kauli
hiyo ya Diamond inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana na pete ya
ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa na ‘kichaa’ huyo wa Bongo Fleva
ambaye amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume
Afrika Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik Magazine
(AFRIMMA) 2014.
Hofu ya kuoa
Akizungumza
na gazeti hili kwenye mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa anahofia
kuoa kwa madai kwamba akifanya hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu
ambacho hataki kimtokee maishani mwake.
Kumbe!
Jamaa
huyo ambaye siku hizi anajiita Dangote (jina la tajiri wa Nigeria, Aliko
Dangote) alitiririka kuwa zamani alikuwa na wazo hilo la kuoa lakini
akiwatazama wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku, makali yao
hupungua na wengine kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.
Bofya hapa kumsikia Diamond
“Unajua unaweza kuona kama vile nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli wenyewe.
“Kuna
wanamuziki wengi walikuwa kwenye peak (kileleni) lakini walipooa tu
‘kiki’ yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine wamepotea kabisa.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
“Ukifuatilia
kwa umakini wapo mastaa wengi duniani ambao umri umekwenda sana lakini
hawajaoa. Hata hapa nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni kuona
kuwa wakifanya hivyo watashuka kimuziki,” alisema Diamond.
Ni kweli kamvisha pete Wema?
Alipoulizwa
kama ni kweli amemvisha pete ya uchumba Wema, msanii huyo hakuwa tayari
kufafanua kwa kigezo kwamba pete ni urembo kama urembo mwingine kwa
mwanamke.
Nje ya boksi
Baada ya
kusikia msimamo wa Diamond, gazeti hili lilijiongeza na kutoka nje ya
boksi ambapo lilizungumza na baadhi ya wasanii waliooa na wasiooa ambapo
walieleza mambo mazito.
Jacqueline Wolper
Siri yafichuka
Katika
mazungumzo yao kwa sharti la kutochorwa gazetini, wasanii hao walidai
kwamba Diamond anahofia kupoteza kiki kwa warembo ambao wengi ndiyo
mashabiki wake wanaoamini nao wanaweza kupata zali la kuolewa naye ndiyo
maana humzingira na kumuomba namba ya simu kila anakokwenda.
Msururu wa mademu
Ilielezwa
kwamba kwa kuwa jamaa huyo hupenda kuwa juu ndiyo maana alisharipotiwa
kutoka na msururu wa wanawake mastaa ambao huchangia jina lake kuendelea
kuwa juu.
Ilidaiwa
kwamba wakati anatafuta namna ya kuchomoka kimuziki alidaiwa kutoka
kimapenzi na warembo waliokuwa na majina madogo kama Rehema Fabian
aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Miss Kiswahili.
Jokate Mwegelo.
Ilisemekana
kwamba baada ya hapo alidaiwa kuwa na msururu wa wanawake mastaa kama
waigizaji Jacqueline Wolper Massawe na Aunt Ezekiel Grayson na Jokate
Mwegelo.
Baadaye
jamaa huyo alidaiwa kuruka na wasichana ambao hawakuwa na kiki hivyo
aliwamwaga ndani ya muda mfupi kama Najma na Natasha.
Baadaye
Diamond alitua kwa Wema hadi akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba
mwaka 2012 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo Masaki jijini Dar.
Kumbukumbu
zinaonesha kwamba muda mfupi baada ya kumvisha Wema pete ya uchumba
walimwagana ambapo Diamond alitua kwa Mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel
Mungilwa ‘Penny’.
Irine Uwoya
Diamond
hakudumu na Penny kwa madai kwamba mrembo huyo hakuwa na kiki kama
ilivyokuwa kwa Wema ambaye jina lake halijawahi kushuka tangu alipovaa
Krauni ya Miss Tanzania 2006/07.
Ilisemekana kwamba hata tuzo zilipungua ndipo akampiga Penny chini na kurudi kwa Wema ambaye inasemekana ndiye anayemng’arisha.
Hawa wameoa, je, wameshuka?
Baadhi ya
mastaa waliooa ni pamoja na Mohamed Ahmed ‘Z-Anto’, Nurdin Bilal
‘Shetta’, Amini Mwinyimkuu, Lawrence Marima ‘Marlaw’, Amani Temba
‘Mheshimiwa Temba’ na wengineo.
Post a Comment