Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wapili kutoka kulia
akipita kukagua matengenezo yanayoendelea ya Kivuko cha MV Kigamboni.
Kulia kwake mwenye kofia ya njano ni Dkt. Wiliam Nsahama Mkurugenzi wa
Huduma za Ufundi (DTES) kutoka Wizara ya Ujenzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe akiendelea na ukaguzi wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe akiwa pamoja na viongozi
wengine kutoka Wizarani na TEMESA wakiwa chini ya Kivuko cha MV
Kigamboni kwa ajili ya Ukaguzi baada ya Matengenezo ya sehemu cha Chini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe akipanda ngazi kuelekea
juu ya Kivuko cha MV Kigamboni kuangalia ukarabati wa sehemu ya juu ya
Kivuko hicho.
Brigedia
Jenarali Rogastian Shaban Laswai akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusiana na maendeleo ya
ukarabati wa Kivuko cha Mv Kigamboni. Wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa.
Luteni
Kanali Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi
Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu uboreshaji wa sehemu ya kupoozea injini ya
kivuko cha Mv Kigamboni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe akipata maelezo kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Post a Comment