Mkuu
wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni
akionesha Kifaa “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha
Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika kusaidia kuwabaini
Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa mengine.
Mkuu
wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni
na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Zanzibar wakionesha baadhi
ya Vifaa Vitalavyotumika kuwachunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia
nchini kutoka mataifa mengine.
Mkuu
wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar Dkt Salma Masauni
akionesha matumizi ya Kifaa cha “THERMAL SCANNER” kwa Wafanyakazi wa
Kituo cha Afya cha Uwanja wa ndege wa Zanzibar. Kifaa hicho kitatumika
kusaidia kuwabaini Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa
mengine.
Na Faki Mjaka Maelezo Zanzibar
Wizara
ya Afya Zanzibar imekabidhi kifaa cha THERMAL SCANNER kwa ajili ya
kuchunguza Wagonjwa wa EBOLA watakao ingia nchini kutoka mataifa
mengine.
Kifaa
hicho kilichowekwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman
Karume kitatumika kwa ajili ya kuwachunguza zaidi Wageni ambao watatoka
katika nchi zilizoathiriwa na Ugonjwa wa Ebola.
Akikabidhi
kifaa hicho Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa Maradhi Zanzibar
Dkt Salma Masauni amesema THEMO SKAN kitasaidia katika kuwabaini watu
ambao wameathirika au kuwa na dalili za Ungojwa wa Ebola na kuchukuliwa
hatua zaidi.
Dkt
Salma amesema iwapo mgonjwa atabainika hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa
ni pamoja na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Chumbuni ambacho
kimetayarishwa kwa ajili hiyo.
Aidha
Dkt Salma amefahamisha kuwa Kituo cha Afya cha Chumbuni kimetengwa kama
eneo litakalotumika kwa ajili ya Matibabu kwa mgonjwa atakayebainika
kuambukizwa Ugonjwa wa Ebola nchini.
Amesema
Wizara ya Afya katika kukabiliana na Ugonjwa huo wa kuambukiza imekuwa
ikifanya Jitihada mbalimbali za kutoa elimu na njia mbali mbali za kinga
kabla ya Zanzibar kuathirika na Ebola.
Amesema
licha ya Vifaa hivyo vilivyotolewa Vifaa vingine vitakuja wiki
inayokuja ili viendelee kutumika katika maeneo ya Bandarini na Viwanja
vya ndege Unguja na Pemba
Dkt.
Salma amesema Ugonjwa huo haujaingia nchini bali Serikali inajiandaa na
juhudi zake za kukabiliana na Ugonjwa huo ili usiweze kuingia na
kuathiri Zanzibar.
Post a Comment