TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16.08.2014.
- KIKONGWE WA MIAKA 80 AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI WILAYANI RUNGWE.
- MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
- MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUANGUKA.
- BWENI MOJA LA SHULE YA SEKONDARI MARANATHA LATEKETEA KWA MOTO.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MATENKI – BODA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA BINADAMU KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
KIKONGWE
WA MIAKA 80 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ADAM MWANDIGA MKAZI WA KIJIJI
CHA KIBISI ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA MOHAMED MWAMELA AMBAYE
ALIKUWA ANAISHI NAYE [MTOTO WA MDOGO WA MAREHEMU].
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA KIBISI, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI WA
KIFAMILIA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA.
MAREHEMU
ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE WENGINE WAWILI AMBAO HAWAKUWEPO WAKATI
TUKIO HILO LINATOKEA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA
MSAKO KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA
MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE
NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. AIDHA ANATOA WITO KWA
WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI NA
UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MPANDA
BAISKELI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA TITO KIWITI (29) MKAZI WA
NYENJELE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA
USAJILI T. 519 AEE AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE MICHAEL KYANDO (27) MKAZI WA MAJENGO – TUNDUMA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA NYENJELE, KATA YA NDALAMBO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA
YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA SUMBAWANGA/TUNDUMA.
CHANZO
CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO
CHA AFYA CHA NYENJELE. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA
MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE
WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA
NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWENDESHA
PIKIPIKI MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FAUTELI SIMFUKWE (65) MKAZI
WA IYUNGA JIJI NA MKOA ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI AMBAYO HAIKUWEZA
KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI AMEFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI HIYO
KUACHA NJIA KISHA KUANGUKA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO EMANUEL SIMFUKWE
(27) MKAZI WA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA AMBAYE ALIKUWA ABIRIA KWENYE
PIKPIKI HIYO ALIJERUHIWA.
AJALI
HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 15.08.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO
ENEO LA MTELEMKO MSANGAMWERU, KATA YA MBALIZI, TARAFA YA BONDE LA
USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MAJERUHI ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA
MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE
WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA
NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA NNE:
BWENI
MOJA LA SHULE YA SEKONDARI MARANATHA ILIYOPO KATA YA IWINDI, TARAFA YA
USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA LIMETEKETEA KWA MOTO JANA
MAJIRA YA SAA 17:20 JIONI.
MWILE
MWAMAHONJE (38) MKAZI WA MARANATHA IWINDI ALIGUNDUA KUUNGUA KWA BWENI
MOJA LA WANAFUNZI LIITWALO ‘MANDELA A’. AIDHA KATIKA AJALI HIYO, MALI
MBALIMBALI ZA WANAFUNZI KAMA VILE VITABU, MAGODORO 30, VITANDA NA SEHEMU
YA JUU YA PAA LILITEKETEA KWA MOTO.
CHANZO
CHA MOTO HUO BADO KUFAHAMIKA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA KWA
MOTO PIA BADO HAIJAFAHAMIKA. MOTO ULIZIMWA KWA JITIHADA ZA KIKOSI CHA
ZIMA MOTO NA UOKOAJI KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI NA WANANCHI.
HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA
MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA TAHADHARI YA
MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KWANI YANA MADHARA MAKUBWA NA YANA SABABISHA
UHARIBIFU WA MALI.
KATIKA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA SADIKI MWANDOLUMA (30) MKAZI WA MATENKI BODA KWA KOSA LA KUSAFIRISHA
BINADAMU KINYUME CHA SHERIA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.08.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA ENEO LA LUBELE, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA
KYELA, MKOA WA MBEYA AKIWA ANAMSAFIRISHA DESTER TAMLATI (24) MKAZI NA
RAIA WA NCHINI ETHIOPIA KINYUME CHA SHERIA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA
MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ZA MTU/WATU AMBAO WANAWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO,WAHAMIAJI
HARAMU NA WENGINEO ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment