Kiongozi: Louis van Gaal alisema mtazamo wa Wayne Rooney ndio sababu ya kumteua kuwa nahodha.
LOUIS van
Gaal amesifu mtazamo wa Wayne Rooney na kuamua kumteua kuwa nahodha wa
Manchester United, lakini amemuonya kujiheshimu nje na ndani ya
uwanja.Mholanzi aliweka wazi kuwa alizungumza na Roonye kuhusu
kumvalisha kitambaa cha umeneja baada ya mechi ya jumanne usiku dhidi ya
Valencia kufuatia mshambuliaji huyo kujituma zaidi kuwa kiongozi.Bosi
wa United alisema: "Nimempa unahodha kwasababu ya mtazamo wake uwanjani
na kwenye uwanja wa mazoezi."
Rooney aliwaongoza mashetani wekundu katika mechi ya kirafiki dhidi ya Valencia siku ya jumanne wii hii.
Anajiamini: Mholanzi huyu amefurahia kumteua nahodha wake kuelekea msimu mpya.
Van Gaal na Rooney wanatarajia kufanya kazi pamoja katika dimba la Old Trafford.
"Sio nje ya uwanja sana, lakini nimemuambia kuwa yeye ni muhimu sana kwangu na amekubali majukumu yake.
"Nilipenda sana jinsi alivyofanya mazoezi na kiwango chake na namna alivyowaongoza wenzake.
"Tukiwa Marekani alifunga magoli mengi na kutoa pasi za mwisho nyingi. Huyu ndiye Wayne ninayemhitaji".
Akizungumza
kuelekea mechi ya kwanza ya Manchester United dhidi ya Swansea kesho
jumamosi, Van Gaal pia alithibitisha kuwa Robin van Persie hana nafasi
ya kucheza.
Aliongeza kuwa Luke Shaw hatacheza mechi hiyo baada ya kuumia na atakaa nje ya uwanja kwa wiki nne.
NA MPENJA BLOG
Post a Comment