Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSAFARA
wa kwanza wa magwiji wa Real Madrid, ‘Real Madrid Legends’ utatua
nchini Tanzania kesho, ukitarajiwa kuongozwa na mwanasoka bora wa zamani
wa dunia na Ulaya, Mreno, Luis Filipe Madeira Figo.
Magwiji
hao watashuka dimbani jumamosi Agosti 23 dhidi ya kikosi maalumu cha
nyota wa zamani wa Tanzania ‘Tanzania All Stars’ ndani ya uwanja wa
kisasa wa Taifa, jijini Dar es salaam.Figo
ataongozana na nyota wengine wawili waliotamba na Real Madrid miaka ya
nyuma, Muingereza Michael Owen na Christian Karembeu.Figo
aliyestaafu soka mwaka 2009, alishinda tuzo mbili mfululizo mwaka 2000
ambazo mwanasoka bora wa Ulya na Dunia na katika enzi zake za kucheza
soka alikuwa mchezaji hatari kupita maelezo na sasa anakuja kukumbushia
ufundi wake katika ardhi ya Rais Jakaya Kikwete.
Mbali
na Figo, mwanasoka mwingine bora wa zamani wa dunia, Zinedine Zidane na
Mbrazil Ronaldo de Lima wanatarajia kutua nchini Ijumaa na kundi kubwa
la magwiji hao.
Mkurugenzi
wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN) (waandaaji wa ziara
hiyo), Farough Baghozah amekaririwa akisema mapokezi makubwa kwa ajili
ya magwiji hao yameandaliwa na watawasili kwa mafungu, lakini kundi
kubwa litaingia nchini Agosti 22.
Baghozah
alisema magwiji hao watapokelewa kwa maandamano kutoka uwanja wa Ndege
wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam na
kupelekwa hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach.
Tayari
kikosi cha ‘Tanzania All Stars’ kimeanza mazoezi katika uwanja wa
Karume jijini Dar es salaam chini ya kocha maarufu, Charles Boniface
Mkwasa ‘Master’akisaidiwa na Fredy Felix Minziro na Jamhuri Kiwhelo
‘Julio’.
Mlinda
mlango na nahodha wa kikosi hicho, Mohamed Mwamweja ametoa wito wa
Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwaona nyota wao wa zamani kwasababu
wamejipanga vizuri.
Mwamweja alikiri kuwa wamekaa muda mrefu bila kucheza mpira, lakini mazoezi hayo yamewaongezea nguvu ya kucheza mechi hiyo.
Kipa
huyo anayetarajia kuanza katika kikosi cha kwanza alisema watajifunza
mengi kutoka kwa magwiji hao, lakini nao watajifunza vitu fulani kutoka
kwa wachezaji wa Tanzania.
Wachezaji wanaoendelea kujifua kwa ajili ya kukumbushia enzi zao na magwiji wa Real Madrid ni:
Makipa waliowahi kutamba nchini Tanzania, Mohamed Mwameja na Peter Manyika.
Watakaosuka
safu ya ulinzi ni mabeki Shadrack John Nsajigwa Mwandemele, Boniface
Pawasa, John Mwansasu, Mecky Mexime, Abubakar Kombo, George Masatu na
Habib Kondo,
Viungo
ni: Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’, Shaaban Ramadhani, Salvatory
Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho Musso, Abdul Mashine,
Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji:
Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel Mwakyusa, Said
Maulid ‘SMG’, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila,
Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka,
Madaraka Suleiman ‘Mzee wa Kiminyio’ na Akida Makunda.
Post a Comment