Ndugu zangu,
Leo
alfajiri niliongoza mjadala kwenye redio za Kwanza Jamii na Nuru FM
kuhusiana na kongamano linaloendelea Dar la Watanzania wa Diaspora
wanaokutana nyumbani, Tanzania.
Ni kwa nini tuna hofu na Watanzania wenzetu walio ughaibuni? Hofu hii ni ya kihistoria.
Kwanini
kongamano hili la kwanza kufanyika lisiwe la mwisho kufanyika katika
sura yake hii, kwamba maudhui ya kongamano yenyewe kuwa ni ; connect,
engage, inform and ivest nako kunakosekana dhana integration kwa maana
ya kujumuisha.
Hoja
kubwa kwa sasa ni kwa namna gani tunawajumuisha wenzetu walio ughaibuni
kupitia uraia pacha. Kwamba wakati umefika wa kubadilika na kuona kuwa
uraia pacha una maanufaa makubwa kwetu kama taifa. Haipaswi kuendelea
kuwachukulia wenzetu walio diaspora kama ‘ Ng’ombe wa Maziwa’- Fuatilia
mjadala huu…
Post a Comment