Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MNIGERIA AMPATIA MASOGANGE PASIPOTI YA SAUZI

 

Agness Gerald ‘Masogange’ akipopzi na Louis Dolnard.
Stori: Sifael Paul na Imelda Mtema
Habari ya mjini kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo ni taarifa kuwa video queen maarufu, Agness Gerald ‘Masogange’ amepatiwa passport (pasipoti) ya kuishi nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara raia wa Nigeria.
MWANAUME KAMWINGIZA MKENGE?

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, ishu hiyo ambayo imekuja miezi kadhaa baada ya ule msala wa Masogange wa madawa ya kulevya ‘unga’ inadaiwa ‘imeinjiniwa’ na mwanaume huyo ambaye haijajulikana kama naye amechukua uraia wa Sauzi au la.
KWA NINI MKENGE?
Ilisemekana kwamba ni mkenge kwa sababu ili Masogange apate pasipoti hiyo, ilibidi aikane nchi yake ya kuzaliwa ya Tanzania. Sheria za uraia wa Bongo kwa sasa zinakataza mtu kuwa na uraia wa nchi mbili.
 
KIKAZI ZAIDI!
Awali, miezi kadhaa iliyopita ilielezwa kuwa Masogange alitimka Sauzi kwa mwanaume huyo ambaye anadaiwa kufanya naye ‘kazi’ (haikutajwa aina ya kazi) nchini humo.
Miezi kadhaa iliyopita Masogange alionyesha kuukataa kabisa Utanzania, baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa kuanzia sasa hataitwa tena Agness, bali umma umtambue kama Thando, jina lenye asili ya watu wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika.
Pia Masogange alitupia mtandaoni picha ya hati yake ya kusafiria ya Sauzi akidai kwamba maskani yake kwa sasa ni kwenye Jiji la Johannesburg nchini humo.Kitendo hicho kinamfanya Masogange ambaye ana asili ya Mkoa wa Mbeya, kuingia nchini kwa viza kama wageni wa mataifa mengine wanavyofanya, wakipewa muda walioomba wa kukaa au kufanya shughuli nyingine yoyote.
Video queen maarufu, Agness Gerald ‘Masogange’ akila ujana na msauzi, Louis Dolnard
Kana kwamba haitoshi, endapo msichana huyo atakumbwa na kosa lolote la kisheria akiwa nchini, anaweza kufukuzwa na kutakiwa kutokuja tena, kama inavyotokea kwa wageni wengine na hivyo kumnyima fursa ya kuwaona wajomba na mashangazi zake walio Mahenge, Kondoa, Mkuranga na maeneo mengine Tanzania.
SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa sheria za Kibongo, Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili (duo citizenship) hivyo Masogange au Thando siyo Mtanzania tena.
MBALI NA MNIGERIA KUNA MSAUZI
Habari ziliendelea kuyeya kwamba mbali na Mnigeria huku, Masogange anadaiwa kuwa na mwanaume mwingine, raia wa Sauzi aitwaye Louis Dolnard ‘anayeminya’ naye nchini humo.
Kwenye Mtandao wa Instagram, mwanadada huyo amekuwa akitupia picha za mahaba niue na mwanaume huyo huku akidaiwa kumsifia jamaa huyo na kumpotezea aliyekuwa mchumba’ke, Evance Komu.
Hii ni picha ya passport ya Afrika kusini ambayo masogange aliitupia instagram.
MASOGANGE ANASEMA?
Akizungumza na gazeti hili, Masogange anayeishi Mbezi-Beach jijini Dar, mara baada ya kukamilisha taratibu za pasipoti hiyo kwenye ubalozi wa Afrika Kusini nchini, mrembo huyo alikiri kukamilisha kila kitu hivyo kukwaa uraia wa nchi hiyo.
Kuhusu mwanaume huyo Mnigeria, Masogange hakuwa tayari kuzungumzia lakini alipoulizwa juu ya yule Msauzi, video queen huyo alikiri kumfahamu huku akigoma kufunguka zaidi.
TUMEFIKAJE HAPA?
Miezi kadhaa iliyopita, Masogange na mwenzake Melissa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na matirio ya kutengenezea madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8 ambapo katika hukumu ya kesi hiyo, staa huyo alitakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela. Yeye alilipa faini hiyo akaachiwa huru.
GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top