Mume wa msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’, Gadner Dibibi akionyesha majeraha baada ya ajali hiyo.
MUME wa
msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’, Gadner Dibibi
amesherehekea Sikukuu ya Idd vibaya baada ya kupata ajali wakati akienda
msikitini.Chanzo cha habari kilitiririka kuwa, Gadner alipata ajali hiyo maeneo ya Mlimani City alipokuwa akishuka kwenye Bajaj ambapo Bodaboda ilimpitia na kumgonga.
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’, Gadner Dibibi wakati wa harusi yao.
“Ameumia
sana, alikuwa akienda kuswali swala ya Idd lakini kwa bahati mbaya
ajali hiyo ikatokea,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina
lake.Gadner alipoatikana alikri kupata ajali hiyo na kueleza kuwa, kwa
sasa anaendelea kuuguza majeraha.
Post a Comment