|
Mwenyekiti
wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa
Bunge Maalumu la Katiba Mhe Samwel Sitta alioowasili kuongoza kikao cha
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika akifuatiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi
Mwenyekiti wa
CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye ukumbi wa NEC
Dodoma ,akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
tayari kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa
CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM
Dodoma.
Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM Dk.Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na mjumbe mwenzake
Samia Suluhu Hassan muda mfupi kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hakijaanza kwenye ukumbi wa NEC mjini
Dodoma.
Katibu wa NEC Oganizesheni Dk.Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Mjumbe
wa Kati Kuu ya CCM DK. Salim Ahmed Salim ndani ya ukumbi wa mkutano wa
White House kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Wajumbe wa
Kamati Kuu ya CCM wakijadiliana kabla ya kuanza kwa kikao kwenye ukumbi
wa NEC mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Profesa Anna Tibaijuka, Katibu wa
NEC Uchumi na Fedha Zakia Meghji na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro.
Naibu Katibu Mkuu
wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Dodoma.(Picha na Adam Mzee)
|
Mwenyekiti
wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu
ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya
CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa CCM
(Visiwani) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein. Kulia ni Makamu wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula
akifuatiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti
wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa katika Uwanja wa
ndege wa Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana, Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wajumbe wa Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel
Nchimbi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama, na Naibu Waziri
wa Fedha na mbunge wa Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Nchemba
on Wednesday, August 20, 2014
Post a Comment