Frank Mvungi_ Maelezo.
Serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi
watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na
Hisabati.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya
Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na
waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
“
Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya
Juu.”Alisema Mwaisobwa.
Akifafanunua,
mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu
wa masomo ya sayansi hapa nchini . Aidha
Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014
ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia
Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na
udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi ambayo ni www.heslb.go.tz.na taarifa hiyo
itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi
ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi
bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa.
WAKATI HUO HUO
WAKATI HUO HUO
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya fedha za
malipo ya mafunzo kwa vitendo kwa mwaka wa masomo 2013 2014.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano
Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.
Mwaisobwa alisema kuwa jumla ya wanafunzi 9946 kutoka vyuo vikuu
vitano hawajapatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ambao wengi wao
tayari wako katika maeneo waliyopangiwa.
“Bodi tayari imeandaa malipo yao na yanatarajiwa kutumwa mwishoni mwa
juma hili, ambapo vyuo vikuu vitano ikiwemo Tumaini Makumira (TUMA)
wanafunzi 1 715, Stefano Moshi (SMMUCO) wanafunzi 1 191, Chuo Cha Usimamizi wa
Fedha (IFM)wanafunzi 2 578, Mt. Augustino (SAUT) wanafunzi 2639 na Teofilo
Kisanji (TEKU) wanafunzi 1823.
Akijibu swali la waandishi wa Habari Mwaisobwa alisema kuwa sababu
zilizopelekea kuchelewa kwa fedha hizo ni mchakato wa upatikanaji wa fedha
zilitarajiwa kupatikana mapema zaidi.
Aidha, Mwaisobwa alitoa rai kwa wazazi na walezi wenye uwezo wa
kuwalipia watoto wao wafanye hivyo ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa
kunufaika na mkopo mkopo wa Bodi.
Post a Comment