Mkuu
wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya Majeshi
Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mkuta huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.
Waandishi
wa Habari kutoka vyombo tofauti wakimsikiliza Bregedia Jenerali Sharif
Sheikh Othman (hayupo pichani) katika Mkutano wake na wandishi leo. Mkurugenzi wa ufundi wa mashindano hayo upande (JWTZ) Luteni Kanali Joseph Bakari akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo.
========== ==========
Na Miza Othman Makame Maelezo- Zanzibar .
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed
Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Michezo ya nane ya
Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itafanyika Zanzibar
kuanzia tarehe 18 mwezi huu.
Akitoa
Taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Makao Mkuu
ya Brigedi Migombani kwa waandishi wa Habari, Mkuu wa Brigedi hiyo
Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman amesema lengo la michezo hiyo ni
kujenga mashirikiano kati ya Majeshi na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema
katika Michezo hiyo kutakuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa na wote
watakuwa washindi, lengo ni kujenga uweledi na nidhamu ndani ya majeshi
yetu.
“Hii
ni fursa ya wanajeshi wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana
pamoja kama tunavyofanya katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi”, alisema
Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman.
Amezitaja
Nchi za Jumuiya hiyo zitakazoshiriki Michezo hiyo kuwa ni wenyeji
Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda. Amesema Michezo
itakayochezwa na wanajeshi hao ni Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira
wa Mikono, Mpira wa Kikapu na Mbio za nyika na ameelezea viwanja
vitakavyofanyika kwa ajili ya michezo hiyo Polisi ziwani ,Vyuo vya
Mfunzo Kilimani, JKU Saateni, Pamoja na Viwanja vya Zimamoto na Uokozi.
Brigedia
Jenerali Sharif Sheikh ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa Michezo
hiyo, amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuona vipaji
vitakavyoonyeshwa na wanajeshi kutoka Nchi hizo .
Akitoa
ufafanuzi wa Michezo hiyo Leftinenti Kanali Joseph Bakari amesema
pamoja na micheo hiyo kutakuwa na Burudani ya Ngoma za Utamaduni kutoka
Vikosi vya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema jumla ya wanamichezo 505 wakiwemo Viongozi kutoka Nchi hizo
watashiriki michezo hiyo itakayodumu kwa muda ya wiki mbili.
Post a Comment