Francis Nanai (kulia) na Tido Mhando (kushoto) wakati wa makabidhiano
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited(MCL), Tido Mhando jana (July 31) amekabidhi ofisi baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na nusu na kampuni hiyo.
Nafasi ya Mhando sasa imechukuliwa na Francis Nanai ambaye hapo kabla alikuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa MCL (CEO) tangu Agosti mwaka jana.
“Mambo yanaendelea vizuri na timu iliyopo ni nzuri ya kuendeleza hapa tulipofikia, nimezungumza mengi na Nanai kama baba na mwanaye, mshikamane, mhakikishe mnafika pazuri zaidi,” Alisema Tido wakati akikabidhi ofisi.
Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL mwaka 2012, Mhando alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kati ya mwaka 2006 na 2010 na kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kati ya 1999 mpaka 2006.
SOURCE: MWANANCHI
Post a Comment