Mwenyekiti
wa Umoja wa Wazazi,Abdallah Bulembo (katikati) akiwasili katika viwanja
vya karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na wasanii
kwenye dua maalum ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki.Kulia
ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve
Nyerere.
Msanii
wa vichekesho ambaye pia ni muinjilisti kwa sasa Emanuel Mgaya Maarufu
kama Masanja Mkandamizaji akiongoza dua kwa upande wa wakristo huku
Msanii Jacob Stephen JB akiwa ameishikilia Biblia.Kulia ni Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum ambaye aliongoza dua kwa
upande wa waislam,katika shuguli hiyo ya kuwaombea Wasanii waliotangulia
mbele ya haki,iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar
es salaam.
Baadhi
ya wadau wa Filamu nchini wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuwaombea Dua
Wasanii wote waliotangulia mbele ya haki (waliofariki) iliyofanyika
kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam jana.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum akijadiliana jambo na baadhi ya wadau walioshiriki kwenye dua hiyo.
Mwenyekiti
wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere akipeana
mkono na watu mbali mbali baada ya kumalizika kwa dua ya kuwaombea
wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika katika viwanja vya
Karimjee,Jijini Dar es salaam.
Post a Comment