Na
Eleuteri Mangi- MAELEZO
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda amewatoa Watanzania hofu
kuhusu suala la wageni kumiliki ardhi nchini.
Waziri
Mkuu Pinda alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano
wa pili wa majadiliano ya pamoja kati ya Serikali ya Mitaa ya China na Tanzania
ambapo walishirikiana pia na sekta ya biashara kutoka nchi hizo.
“Hofu
ni halali na ni lazima kwa Watanzania katika masuala ya umiliki wa ardhi maana
ni vema tuifikishe nchi mahali pazuri” alisema Pinda. Waziri
Mkuu Pinda alisema kuwa Tanzania ni nchi inayolinda ardhi yake tofauti na nchi
nyingine ambapo ardhi yote ni mali ya umma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ndio mwenye dhamana na mamlaka na ardhi ya Tanzania kwa niaba ya
Watanzania.
Akifafanua
Waziri Mkuu alisema kuwa suala la mwananchi au mwekezaji kumiliki ardhi
hutolewa kwa kipindi kwa maalumu kwa minajili ya kutoa huduma mbalimbali za
kijamii ambapo mwekezaji anapewa umiliki wa ardhi kwa muda tofauti kulingana na
huduma anayotoa. Waziri
Mkuu Pinda alisema kuwa Watanzania ni lazima wajipange vizuri ili kuifikisha
nchi mahali pazuri katika masuala ya uwekezaji ambapo nchi haiwezi kuendelea bila
kuwa na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
“Ushirikiano
tunaoufungua na rafiki zetu kutoka China ni hatua kubwa ya kutambua na
kusimamia dira yetu kati ya Tanzania na
China ambayo ni kielelezo cha malengo makubwa ya mataifa haya mawili kwa
kuzingatia uwekezaji unaojali usalama wa mazingira na kuboresha maisha ya watu”
alisema Pinda.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Hawa Ghasia akimkaribisha Waziri Mkuu alisema kuwa sekta binafsi na
uwekezaji nchini na China zinasaidia kuongeza fursa za biashara na uwekezaji
baina ya nchi hizo mbili na zitasaidia kukuza kipato cha wananchi na nchi kwa
ujumla.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini akitoa mada juu ya fursa za
uwekezaji alisema kuwa Tanzania ina maeneo mengi yenye fursa za kiuwekezaji. Sagini
aliyataja maeneo hayo kuwa ni mikoa 8 ikijumuisha Tanga, Dar es salaam, Pwani,
Morogoro, Mtwara, Lindi, Katavi na Singida.
Post a Comment