Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ akiwacharukia wanaume waliokuwa wanampigia miluzi huku wakimzodoa.
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’
hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa
amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.
‘Amanda’ akiingia kwenye gari kuondoka
Tukio hilo lililowashangaza wengi
lilijiri eneo la Mwenge Bamaga jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa
akitembea kuelekea kwenye mgahawa uliopo eneo hilo.
Huku akitembea kwa staili ya
‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani
kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza
mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume
ambao wengi wao ni madereva wa Bajaj na mafundi gereji walionekana
kumzodoa huku wakieleza kuwa, ni msanii asiyejiheshimu.
“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo nini?
Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale
wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa
tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.
Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni
hicho, mwandishi wetu alimfuata Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote
aliingia kwenye gari na kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara
waliokuwa wakimpigia miluzi. Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila
kupokelewa.
Post a Comment