Kundi
la wapiganaji wa Kiislamu la Iraq na Syria (ISIS) limetekeleza mauji
mengine ya kutisha kwa kumkata kichwa mwandishi mwingine wa habari wa
Marekani.
Mwandishi
huyo aliyetajwa kwa jina la Steven Sotloff mwenye umri wa miaka 31
alitekwa na wapiganaji hao mwezi August mwaka jana.Mwezi uliopita
Sotloff alionekana mwishoni katika picha za video zilizoonyeshwa
kuhusiana na kuchinjwa kwa mwandishi mwingine wa Marekani James Foley.
Katika video hiyo iliyopachikwa hapo chini, mwandishi huyu anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.
Sotloff ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa:
'Obama,
your foreign policy of intervention in Iraq was supposed to be for
preservation of American lives and interests, so why is it that I am
paying the price of your interference with my life?.''
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kiingereza anamlaumu Rais Obama kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
“I’m back, Obama, and I’m back because of your arrogant foreign policy towards the Islamic State..
“As
your missiles continue to strike our people, our knife will continue to
strike necks of your people,” anasikika akisema kabla ya kutekeleza
kitendo hicho cha kikatali.
Muuaji huyu anasadikika kuwa ni yule yule aliyemchinja mwandishi wa kwanza mwezi uliopita.
Punde baada ya kukamilisha hotuba yake,muuaji huyo anaanza kumchinja Sotloff lakini video hiyo inazimwa .
Sekunde
chache baadaye mateka mwingine raia wa Uingereza David Cawthorne
Haines, anaonekana kabla ya ilani kutolewa kuwa hatima yake iko mikononi
mwa taifa la Marekani.
Tazama
Video hapo chini( Video inatisha) .Video hii imeanza na hotuba
fupi ya Rais Obama . Baada ya hotuba hiyo, Mwandishi huyo
anawekwa mbele ya kamera na kuuawa kikatili.
Post a Comment