Wakati
wimbo wa MdogoMdogo ukiwa bado unasumbua kwenye media, Diamond
Platinumz anatarajia kurusha mawe mengine mazito zaidi kwa ajili ya
kuwaburudisha mashabiki wake.
Akiongea
na tovuti ya Times Fm, Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond amesema
mkali huyo anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa mpigo na kwamba zote
zimetayarishwa nje.
“Tusubirie kidogo, baada ya
miezi miwili mitatu tutaongea kwa sababu kuna kazi zinakuja, Diamond
anarelease ngoma mbili mfululizo na zote zimetoka nje. Lakini hatuwezi
kueongea sasa hivi hadi muda ufike.” Babu Tale ameiambia tovuti ya Times
Fm.
Inaonekana Diamond hataki
kuacha gap, anakandamizia palepale azidi kwenda juu na kutwaa tuzo
nyingi za kimataifa kama alivyofanya mwaka huu.
Endelea kusubiri, tutakujuza hapa hapa..
Post a Comment