Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemhukumu kwenda jela miaka 30 mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Mbwawa Steven Solomon (29) kwa kosa la kumbaka mfanyakazi wake wa nyumbani mwenye umri wa miaka 16.
Akitoa
hukumu hiyo Hakimu wa mahakama hiyo, Harieth Mwailolo alisema
iliridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa chini ya
mwendesha mashitaka Salim Msemo.
Ilielezwa
kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 30 mwaka huu huko Mbwawa
Mtongani Kata ya Kilangalanga Tarafa ya Mlandizi wilayani Kibaha.
Mlinzi huyo alifanya unyama huo wakati mkewe akiwa amelazwa Kituo cha Afya cha Kilangalanga.
Mahakama
ilielezwa kuwa mtuhumiwa baada ya kufanya tukio hilo alikutwa na mjumbe
wa shina namba 13 Kilangalanga, Mwajuma Rajabu na mashahidi wengine na
mlalamikaji na kukubaliana kuwa atamlipa kiasi cha Sh milioni moja kwa
ahadi ya kila mwezi angetoa kiasi cha Sh 70,000 makubaliano ambayo
yalifanywa Aprili Mosi mwaka huu.
Mlinzi
huyo alijutia kosa alilofanya na kuiomba Mahakama kumpunguzia adhabu
hata hivyo Mahakama iliamuru atumikie kifungo cha miaka 30 jela.
Post a Comment