Mtangazajiwa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.
Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva
alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake
huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia
kutengana kwao.
“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto
na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume
nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu
kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea
tu,” alisema Diva.Akaongeza:
“Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi,
mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni
mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”
Diva alikwenda mbele zaidi
kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha
Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’
na mtangazaji Salama Jabir.
Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.
Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya
Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya
kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi
kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao
kwa sababu atachafuka kisiasa.
E-mail ilisomeka hivi:
“Unanikosea sana ujue
unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa kiongozi kwa
sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.
“Ungekuwa unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara
tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea
sanasana.”
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.
Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.
Kufuatia Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya
mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi
wake, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na
mtangazaji huyo.
Wengi walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi
kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.
“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye
vyombo vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya,
Jackson Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa
huyo, Huddah Monroe.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.
Kufuatia madai hayo, kwa muda wa
siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa njia ya simu lakini bila
mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa alipo, walisema wanachojua
ana shughuli zake nchini Zambia.
Chanzo: Amani/Gpl
Post a Comment