Daktari
wa midundo, Dr Dre ameongoza orodha ya Forbes ‘Hip Hop Cash Kings 2014’
akivaa taji hilo baada ya kuingiza kiasi cha $620 million mwaka huu.
Sio tu kwamba Dr Dre ameongoza orodha hiyo bali ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa kiwango alichoingiza kinazidi jumla ya fedha zote walizoingiza wasanii wengine 24 walioingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Dre anarudi kwenye nafasi yake hiyo aliyokuwa akiishikilia mwaka 2012 kabla ya kufunikwa na P. Diddy mwaka jana.
Sio tu kwamba Dr Dre ameongoza orodha hiyo bali ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa kiwango alichoingiza kinazidi jumla ya fedha zote walizoingiza wasanii wengine 24 walioingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Dre anarudi kwenye nafasi yake hiyo aliyokuwa akiishikilia mwaka 2012 kabla ya kufunikwa na P. Diddy mwaka jana.
Nafasi ya pili imeshikiliwa na Jay Z na P.Diddy ambao wamefungana kwa kuingiza kiasi cha $60 million kila mmoja.
Jay Z ameingiza kiasi hicho kupitia matamasha mengi aliyoyafanya, biashara zake na album yake ya Magna Carter Holy Grail iliyofikia mauzo ya Platinum hata kabla haijaachiwa baada ya kampuni ya Sumsang kununua nakala milioni moja.
P. Diddy yeye aliingiza kiasi hicho ($60 million) kupitia biashara zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wake wa mavazi wa Sean Jean, Revolt TV na mengine.
Rapper wa Young Money, Drake anashikilia nafasi ya 4 katika orodha hiyo akiwa ameingiza kiasi cha $33 million. Kiasi hiki kimetokana na mauzo ya album yake ya ‘Nothing Was The Same’ iliyouza nakala zaidi ya Milioni 4 duniani kote. Kiasi kingine kiliigia kupitia endorsement ya Jordan na tour yake.
Nafasi ya 5 imeshikiliwa na wasanii wanaofanya kazi pamoja Macklemore & Ryan Lewis ambao wameingiza kiasi cha $ 32 million. Wasanii hao walifanikiwa mwaka jana kushinda tuzo nne za Grammy kati ya saba walizokuwa wakiwania. Ushindi huo uliwasaidia kupata shows nyingi zaidi na kufanya biashara kubwa mtaani.
Kanye West amekamata nafasi ya 6 akiwa ameingiza kiasi cha $30 million. Tour yake ya ‘Yeezus’ ilifanikiwa zaidi na kumuingizia kipato kikubwa na kumsaidia kuongeza pato la mwaka kwa asilimia 50.
orodha kamili:
1. Dr Dre- $ 620 Million
2. Jay Z- $60 Million (tie)
3. Diddy- 60 Million (tie)
4. Drake – 33 Million
5. Macklemore & Ryan Lewis 32 Million
6. Kanye West- 30Million
7. Birdman – 24Million
8. Lil Wayne- 23Million
9. Pharell William -22Million
10. Eminem- 18Million
11. Nicki Minaj- 14Million
12. Wiz Khalifa- 13Million (tie)
13. Pitbull- 13Million (tie)
14. Snoop Dogg- 10Million
15. Kendrick Lamar- 9Million
16. Luda Cris – 8Million (tie)
17. Tech N9ne- 8Million (tie)
18. Swizz Beatz -8Million (tie)
19. 50 Cent- 8Million (tie)
20. Rick Ross- 7Million (tie)
21. J. Cole –7Million (tie)
22. DJ Khaled- 7Million (tie)
23. Lil Jon- 7Million (tie)
24. Mac Miller -7Million
Post a Comment