Na Benedict Liwenga na Magreth Kinabo, Maelezo-Dodoma.
KAMATI za Bunge Maalum la Katiba leo tarehe 4 Septemba, 2014 zimeendelea kuwasilisha taarifa zao mbele ya Bunge hilo.
Baadhi ya kamati zilizowasilisha taarifa zao katika Bunge hilo ni Kamati
Namba Mbili, Kamati Namba Tisa, Kamati na Kumi, Kamati Namba Nne,
Kamati Namba 12, ambazo ziliwasilisha asubuhi hadi mchana.
Mambo
makubwa yaliyozungumzwa katika Bunge hilo yanahusu mambo mbalimbali
yakiwemo ya Uongozi wa Bunge, ambapo wengi wapendekeza wabunge wanaweza
kuchaguliwa Spika au Naibu Spika na Mbunge kutowajibishwa na wananchi.Pia kigezo cha kugombea nafasi ya ubunge kikiwa ni kujua kusoma na kuandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Katika
uwasilishaji huo, Kamati Namba Nne ya Bunge hilo, iliwasilisha taarifa
yake, ambayo ilisomwa na Gosbert Blandes, taarifa, ambapo katika Ibara
ya 132 inahusu Spika na Mamlaka ya Spika.
Wajumbe
wengi wanapendekeza ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kwa kumwondoa
mbunge kuwa miongoni mwa watu wasioruhusiwa kushika madaraka ya Spika.
Aidha
siku za kuwasilisha tamko rasmi kuhusu mali zimeongezwa kutoka siku
thelathini hadi tisini. Ibara hiyo ndogo ya (2) sasa itasomeka kama; (2)
Waziri, Naibu Waziri, Mbunge au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine
yoyote yatakayotajwa na sheria za nchi kwa madhumuni ya Ibara hii,
hataweza kuchaguliwa kuwa Spika.
Sababu
za mapendekezo ni kumwezesha Mbunge kugombea nafasi ya Spika na
kuongeza siku za kuwasilisha tamko rasmi kuhusu mali ili kuondoa
uwezekano wa Spika kushindwa kufanya hivyo kutokana na ufinyu wa muda.
Ibara
ya 133, ibara hii inahusu ukomo wa Spika. Baada ya mjadala Wajumbe
walio wengi walipendekeza kufanya marekebisho kwa kufuta aya ya (a)
linaloweka sharti la kukoma kwa nafasi yake kutokana na kuchaguliwa kuwa
mbunge. Sababu za mapendekezo haya ni kutoa fursa kwa wabunge kushika
madaraka ya Spika na kuendelea kushikilia nafasi zao za ubunge.
Ibara
ya 134, ibara hii inahusu Naibu Spika. Kamati imejadili kwa kina ibara
hii kasha wajumbe walio wengi walikuwa na mapendekezo kuwa ibara
ifanyiwe marekebisho kwa kuondoa neno Mbunge katika Ibara ndogo ya (2).
Ibara hiyo sasa itasomeka kama ifuatavyo; 134 (2) Waziri, Naibu Waziri
au mtu mwenye madaraka ya aina nyingine yoyote yatakayotajwa na sheria
za nchi kwa madhumuni ya Ibara hii, hataweza kuchaguliwa kuwa Naibu
Spika. Sababu za mapendekezo haya ni kuwawezesha Wabunge kuwa na sifa ya
kuchaguliwa kuwa Spika.
Ibara
ya 135, Ibara hii inahusu sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu
Spika. Kamati imejadili kwa kina kuhusu sifa za mtu kuchaguliwa kuwa
Spika au Naibu Spika. Baada ya mjadala wajumbe walio wengi walipendekeza
kuifanyia marekebisho ibara hii. Lengo la marekebisho haya ni kutoa
wigo mpana kwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwa na haki
ya kuchaguliwa kuwa Spika na Naibu Spika ilimradi wana shahada ya Chuo
kikuu inayotambulika. Ibara hii sasa itasomeka kama ifuatavyo;
135
(1) (1) Mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika endapo mtu
huyo ana elimu ya shahada ya chuo cha elimu ya juu kinachotambulika kwa
mujibu wa sheria za nchi; (2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo
ya (1), mtu atastahili kuchaguliwa kuwa Spika au Naibu Spika ikiwa ana
sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mbunge.
Kamati
Namba Kumi ya Bunge Maalum nayo iliwasilisha taarifa yake kuhusu
sura ya Rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa sura ya tisa na sura
ya kumi, ambayo ilisomwa na Dk. Dalaly Kafumu.
Dk.
Kafumu alisema katika suala la Uchaguzi wa wabunge, Ibara ya 124(4) ya
Rasimu ya Katiba inazungumzia uchaguzi wa mbunge endapo kiti cha ubunge
kipo wazi.
“Kamati
yangu inaona kuwa ibara hii inalenga kufuta uchaguzi mdogo kwa kuwa
ibara hii inatoa mwanya wa mtu kuteuliwa na kutangazwa na Tume ya
Uchaguzi, kutoka kwenye orodha ya majina ya wagombea iliyowasilishwa kwa
Tume Huru ya Uchaguzi.
“Kamati yangu haikubaliani na utaratibu huo, hivyo inapendekeza
kwa utaratibu unaotoa haki ya mtu kugombea na kuchaguliwa kama ilivyo katika ya sasa,” alisema.
Utaratibu
wa kutayarisha orodha ya majina uliotajwa katika ibara ya 124 wa
kumpata mbunge haujawekwa bayana kwa maana ya kuainisha mfumo wa uwiano
wa kura na idadi ya wagombea kwani inatakiwa kuwa sawa na idadi ya viti
bungeni. Aidha, mfumo unaopendekezwa utaleta dhana ya “Mbunge mtarajiwa”
hali inayoweza kuathiri demokrasia na hata utendaji wa kazi wa mbunge
anayekuwa madarakani. Kutokana na sababu hizo, Wajumbe wamependekeza
ibara ndogo ya (4) ifanyiwe marekebisho na kusomeka; “(4) Endapo Mbunge
anayetokana na chama cha siasa atapoteza sifa za kuwa Mbunge kwa sababu
yoyote isiyokuwa ya Bunge kumaliza muda wake, Tume Huru ya Uchaguzi
itatangaza uchaguzi wa Mbunge katika Jimbo hilo, kwa mujibu wa masharti
ya Katiba hii”.
Alisema
katika Ibara ya 125 (1) b kuhusu sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge kuwa
elimu isiyopungua kidato cha nne. Wajumbe walio wengi wamekubaliana kuwa
ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kwa kuondoa kiwango cha elimu kwa kuwa
suala la kugombea nafasi yoyote ni la kidemokrasia, haipaswi mtu kuzuiwa
kugombea kwa kigezo cha elimu, kwani ni haki ya Katiba.
“Hali
kadhalika, Katiba haitakiwi kuweka kigezo chochote kinachokiuka haki za
msingi za kuchaguliwa na kuchagua. Pili haki ya kuamua kama mgombea
anafaa au hafai ni ya wapiga kura,wasizuiwe kikatiba kutumia haki yao ya
msingi ya kuchagua mtu wanayemtaka. Pia utaratibu huuu haupo duniani
kote hata kwa nchi zilizona demokrasia iliyokomaa,” alisema Blandes.
Aliongeza
kuwa wajumbe walipendekeza Ibara hiyo ifanyiwe marekebisho kwa
kuweka cha kujua kusoma na kuandika na si kiwango cha elimu kama sifa ya
msingi.Hivyo isomeke ifuatavyo:
“(1) (b) Anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.”
Aidha Dk. Kafumu aliongeza kuwa katika Ibara ya 129 kuhusu haki ya wapiga kura kumwajibisha Mbunge .
“Wajumbe
wengi wamependekeza kuwa, wapiga kura watumie haki yao ya kumwajibisha
mbunge kwa njia ya kidemokrasia ya kupiga kura kila baada ya kipindi cha
miaka mitano kinapokwisha. Kamati imeona kuwa, kwa kadri demokrasia ya
vyama vingi inayoendelea kukua, upo uwezekano wa watu wachache kuweza
kutumia mbinu hasi kumuondoa mbunge anayefaa bila ya kuwa na sababu za
msingi. Hivyo basi wajumbe walio wengi wamependekeza ibara hii ifutwe
yote.
Wakati
kwa upande wa maoni ya walio wachache, ambayo yalisomwa na Dk. Tulia
Ackson, ambapo alisema katika Ibara 124 inayohusu uchaguzi wa wabunge ,
walitofautiana na walio wengi kwa kusema kuwa inajitosheleza.
“Hii
Ibara ni muhimu ibaki kama ilivyo kwani inapunguza matumizi makubwa ya
fedha ambayo yameshuhudiwa na wananchi,” alisema Dk. Tulia.
Aliongeza
kwamba katika Ibara ya 129 walitofautiana na wajumbe wali wengi kwa
kusema kuwa ibara hiyo inajitosheleza kwani iwapa wananchi haki ya
kuweza kumwajibisha mbunge ambaye hawajibiki ipasavyo katika
kuwawakilisha wananchi na kuwatafuatia wananchi ufumbuzi wa matatizo
yao.
Wajumbe walio wachache walipendekeza ibara hiyo ibaki isipokuwa irekebishwe kama ifuatavyo:
129
(1) Bila kuathiri masharti ya Katiba hii, wananchiwatakuwa na haki ya
kumwondoa Mbunge wao madarakani, endapo Mbunge atashindwa kuwasilisha
aua kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake.
(2)Bunge
litatunga sheria kuweka masharti ya kuendesha uchunguzi kwa mbunge
atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapiga kura wake na
utaratibu wa kumwondoa katika Ubunge.
Post a Comment