Mwanaume
mmoja mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini Mwanza amekutwa amekufa
baada ya kujinyonga kwa kamba juu ya mti huku mwili wake
ukiwa umeharibika vibaya na kuvuja maji….
Inakadiriwa
kuwa mtu huyo alijinyonga siku tatu zilizopita na chanzo cha
kifo hicho bado hakijafahamika kutokana na mtu huyo kutoaacha
ujumbe wowote huku wakazi wa eneo hilo wakishindwa kumtambua
vizuri kutokana na mwili wake kuharibika.
Kutokana
na hali hiyo, maafisa wa jeshi la polisi waliokuwepo eneo la
tukio waliamuru mwili huo uzikwe baada ya uchunguzi wa awali
wa daktari aliyekuwepo eneo la tukio.
Zoezi la kutoa mwili wa marehemu kutoka kwenye mti likiendelea
Post a Comment