Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Madee atoka nje kwa dhamana baada ya kuhusishwa na tukio la utekaji


Muimbaji wa Tip Top Connection, Madee hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuwekwa ndani katika kituo cha polisi cha Kigamboni kutokana na madai ya kuhusishwa na tukio la utekaji.
 
Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo, Babu Tale, mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown aliripoti kupitia ‘You Heard’ ya XXL kuwa Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni
 
Babu Tale alisema: "Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora,kwahiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki halafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma.
 
"Pikipiki ilivyodondoka yule aliyekua nyuma kwenye pikipiki ambaye ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliyekuwa anaendesha hiyo pikipiki.
 
“Wakamchukua na kwenda nae maskani TipTop,” ameeleza Tale. 
 
Mama yake akaja akasema,"msipeleke polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu. Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake, saa nne asubuhi yule mama akaja na polisi badala ya kuja na mwizi, mwenzake akaja na polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop.
 
" Walimchukua huyo mhalifu kwenye Land Rover mpaka Polisi Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa.”
 
“Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka hospitali. Nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa polisi akaripoti, kufika kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka hospitali akawaambia ‘huyu ni mwizi ameiba’ Ikabidi dogo aingizwe ndani jana akalala pale polisi Magomeni.
 
“Asubuhi yake Madee akaenda kituoni kama kufuata mhalifu wake na kutaka simu yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe Kigamboni. Saa kumi na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia meseji anasema Madee analalamika mbona humfatilii, nikauliza ‘kuna nini tena’ akasema wamemuingiza ndani. 
 
"Nikapiga simu polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako tulitaka kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu. Nikapiga simu kwenye vyanzo vyangu vya msaada tukamtolea dhamana, ni hilo, yataisha kama yalivyoanza"-Babu Tale
 
Source:Millardayo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top