Mahakama Kuu ya Tanzania iliyokaa chini ya Majaji Augustine Mwarija,
Aloysius Mujulizi na Dr Fauz Twaib imetoa uamuzi wake kufuatia
maombi ya Saed Kubenea kama ifuatavyo;
1.Kuna mgongano mkubwa kati ya toleo la Kiswahili na Toleo la
Kiingereza la kifungu cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
2. Kwamba pamoja na mgongano huo, Sheria imekusudia kwamba Madaraka
ya Bunge Maalum la Katiba yatatekelezwa kupitia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya katiba
kama ilivyowasilishwa kwake.
3. Kwamba mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba yana mipaka, na kwamba madaraka yake
yanaongozwa na kutekelezwa kupitia Rasimu. Bunge Maalumu la Katiba linaweza kubadili na
kuboresha mapendekezo yaliyomo katika Rasimu mradi tu maboresho yasiende
kinyume na misingi iliyowekwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya katiba,
kama ilivyokuwa pia kwa Tume.
4.Mahakama Kuu haina Mamlaka ya kuamua ni kiwango gani Bunge maalumu la Katiba linaweza kuboresha Rasimu kwani hilo ni suala la kisiasa, ingawa Bunge Maalumu la Katiba linafungwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya katiba.

Post a Comment