MSICHANA
Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini Dar, ambaye mguu wake mmoja
umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo 75 na kumsababishia maumivu
makali, anahitaji kiasi cha shilingi 5,000,000 ili aweze kufanyiwa
upasuaji nchini India.Msichana Zuhuru Juma (27) mkazi wa Temeke jijini
Dar, ambaye mguu wake mmoja umevimba kiasi cha kufikisha uzito wa kilo
75. Uvimbe huo unaomfanya alie kila mara uliifanya Kampuni ya Global
Publishers kwa kushirikiana na Kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha DTV, kuwasiliana na daktari aitwaye Sabapathy wa India, aliyekubali kuifanya kazi hiyo kwa kiwango hicho cha fedha, tofauti na madai ya awali kuwa zingehitajika shilingi milioni 30.

Daktari huyo ambaye pia alimtibia mtoto Hamisi aliyekuwa na matatizo
kama hayo ambaye hali yake inaendelea vyema, alisema msichana huyo
atarejea katika hali yake ya kawaida endapo ataweza kufika hospitalini
kwake na kumpangia kwa ajili ya upasuaji hapo Oktoba 25, mwaka huu.
Zuhura amewaomba Watanzania kumsaidie ili kuweza kupata matatibu hayo
aweze kupona na kuendelea kuwalea watoto wake ambao ni wadogo
wanaohitaji msaada wake kama mama na kwamba aliyeguswa na tatizo
linalomkabili anaweza kumsaidia kupitia simu yake ya mkononi namba
0717319555.
Post a Comment