Washiriki
wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 walitoa misaada ya kijamii
katika Hospitali za Misheni Kilema na ile ya K.K.K.T Marangu baada ya
kutembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Mwakilishi wa Kanda ya Ziwa katika Shindano la Redds
Miss Tanzania 2014 Dorine Robert akimpa zawadi ya chandarua mgonjwa Jamila
Msafiri aliyelazwa katika Hospitali ya Kilema Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani
Kilimanjaro jana ambapo warembo 30 wa Miss Tanzania walitoa msaaada mbalimbali
ya kijamii hospitalini hapo.
Warembo waiangalia watoto
picha ya pamoja ya warembo na wenyeji Hospitali ya Kilema Moshi.
Hapa ni Hospitali ya KKKT Marangu.
Mpigapicha wa True Vision John Lymo akiwajibika kwa kuakama taswira za warembo.
Baada
ya hapo warembo na viongozi walishirikki chakula cha mchana nyumbani kwa
Naibu Kamanda wa UVCCM Moshi Vijijini, Innocent Shirima Melleck.
Washiriki
wa Shindano la Redd's Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Afisa Mfawidhi,
Nisalile Mwangoka aliyekuwa akiwapa maelezo juu ya upimaji wa wageni
wanao ingia nchini kupitia viwanja vya ndege unavyofanyika kutumia
mashine maalum iitwayo 'Walk Through Thermoscaner', iliyopo uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati warembo 30 wanaowania
taji la Miss Tanzania walipotembelea uwanja huo na kujifunza mambo
mbalimbali . Warembo hao wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa
ndani kwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.
Mashine hiyo ikionekana kufungwa juu kuelekea usawa wa kuingilia abiria wanaowasili tka nje ya nchi.
Namna inavyoonekana baada ya kipimo kuchukuliwa
Nisalile
Mwangoka akionesha kifaa cha zamani cha upimaji ugonjwa wa Ebola
ambacho kimeelezwa kuwa licha ya ufanisi lakini kilikuwa kinaweka foleni
kwa abiria tofauti na hicho kipya.
Meneja
wa Usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),
Kisusi Makomondi akiwapa maelezo washiriki hao wa shindano la Miss
Tanzaniua 2014 juu ya shughuli mbalimbali za uwanja huo.
Warembo wakianza ziara
Camera man wa True Vision John Lymo akiwajibika uwanjani KIA.
Warembo pia walipata fursa ya kutembelea kikosi cha zima moto uwanjani hapo.
Warembo hao baada ya kutembelea Uwanja wa Ndege KIA waliwasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Mkuu
wa Wilaya (DC) wa Arumeru, Nyirembe Munassa Sabi,akiwa na warembo
baada ya kuwapokea ambapo walitarajiwa kufanya ziara ya kutembelea
vivutio vya utalii hifadhi ya Arusha na Namanga katika mpaka wa Tanzania
na Kenya.
Post a Comment