Mez B amejitetea kwa kusema kuwa alilazimishwa kupiga picha hizo na maboyfriend wa wasichana hao ambao ni wazungu.
“Zile picha bwana dah hata mimi nimesikitika pia… mi nilikuwa nashoot video…sasa kuna wadada wawili walikuwa wanaoga kwenye swimming pool na maboyfriend zao wazungu Mikadi na walikuwa vifua wazi tu vile vile, sasa mwisho wa picha wakaomba kupiga picha. Actually mimi nilikataa kwa style ile, mwisho wa siku wakaja na maboyfriend zao wakawa wananilazimisha please please just do it just do it bana picha tu, director wangu mwishoni akasema ngoja tupige tu tuwaridhishe then si tunazifuta”. Amesema Mez B kupitia MTANDAO MAKINI WA PAPARAZI.
Mez B ameongeza kuwa tukio hilo lilitokea mwaka jana mwishoni na hajui ni nani ambaye amezivujisha picha hizo.
“Ni muda sana yaani hizo picha ni za mwaka jana mwishoni mwezi wa 12 nilipokuwa nashoot video ya shemeji, kwahiyo sasa nimeshangaa hizo picha hazikufutwa na zimesambaa na hata director mwenyewe nimemuuliza yeye mwenyewe anashangaa na kwasababu kuna dogo mmoja alikuwa anafanya nae pale kazi wakagombana, yule dogo aliondoka kwahiyo akawa anamuhisi huyo dogo atakuwa ndio amezivujisha.
Director mwenyewe anasema sio yeye ofcourse ni mtu na heshima zake yaani”.
Post a Comment