Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mfanyabiashara mwingine tena afia GESTI Jijini Arusha


Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Olais Metili mkazi wa Uzunguni jijini Arusha, amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ya Hoteli Diamond Motel iliyopo eneo la Sakina jijini hapa.
Mwili wa mfanyabishara huyo anayemiliki mali mbalimbali ikiwamo mgahawa wa Bite Bite na duka maarufu la vinyago eneo la Kisongo uligundulika jana saa 7:00 mchana, wakati wahudumu wa hoteli hiyo wakitaka kufanya usafi chumba alichokuwa amepanga.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri unaokadiriwa kufikia miaka 56 , ilidaiwa aliingia hotelini hapo na mwanamke mmoja ambaye hata hivyo, haikujulikana muda ambao alitoka.
“ Metili (Marehemu) alifika katika hoteli hiyo akiwa ameongozana na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika na kuingia katika chumba chake na haijulikani aliondoka muda gani huyo mwanamke,”alisema mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana jana kuelezea taarifa za awali za uchunguzi wa kifo hicho, lakini maofisa wa polisi waliuchukua mwili huo, wakisema huenda kesho taarifa itatolewa rasmi.
Tukio hili, linakumbusha kifo cha Kada wa CCM, Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa, Benson Mollel ambaye alifariki dunia katika hoteli ya Lash Garden eneo la Jakaranda ambapo pia alidaiwa aliingia katika chumba hicho na mwanamke.
Matukio ya kufa katika nyumba za wageni, katika jiji la Arusha, yanahusishwa na matumizi ya pombe kali au dawa za nguvu za kiume kwa wanaume wengi ambapo dawa zimekuwa zikiuzwa katika maeneo mengi jijini hapa bila ya udhibiti mkali
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top