Nuru Ramadhani
Nasibu (pichani), mkazi wa jijini Dar es Salaam aliyekuwa akitafutwa na
polisi wa nchini na wa kimataifa (Interpol) kwa kuhusishwa na wizi wa
kuaminiwa wa magari matatu mali ya Dk. Emmanuel Matech ametiwa mbaroni.Taarifa
zilizopatikana ndani ya jeshi hilo juzi zinadai mwanamke huyo alitiwa
mbaroni hivi karibuni na kwa sasa jalada la kesi yake linaandaliwa
kwenda kwa mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) kwa hiyo yupo nje kwa
dhamana.
Kabla ya kutiwa mbaroni kwa
mwanamke huyo ambaye ni mke wa kigogo wa ulinzi wa kampuni ya taasisi
moja ya umma nchini, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni
kwa kupitia ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai liliandika
barua Julai 13, mwaka huu iliyokuwa na namba ya jalada OB/IR/5705//2014 wizi wa kuaminiwa.
Katika barua hiyo, magari
matatu yalitajwa kuibwa kwa kuaminiwa na mwanamke huyo ambayo ni Toyota
Harrier (namba T 948 CGV), Toyota Prado (T 928 CJS) na Toyota Rav 4 (T
673 BXR) na mtuhumiwa ametajwa kwamba ni Nuru ambaye alikuwa bado
hajakamatwa.
Tangazo la kumsaka mwanamke
huyo lilitolewa baada ya Dk. Matech kutoa taarifa polisi na kufungua
kesi yenye jalada namba OB/RB/10649/2014 wizi wa kuaminika, mtuhumiwa
akiwa Nuru.Mwandishi wa habari hii alimtafuta mmiliki huyo ambaye katika
mahojiano alikiri kuwa magari hayo ni yake lakini Nuru alikwenda kwake
Januari, mwaka huu na kukodisha kwa awamu tofauti ambapo awali alilipa
na aliamini angeyarudisha kwa muda waliokubaliana lakini hakufanya
hivyo.
“Kilichoniumiza moyo ni pale
nilipomfuatilia ili anilipe fedha zangu na magari yangu, alinipa cheki
ya Februari 8, mwaka huu, ya shilingi milioni tano, kwenda Benki ya NMB
lakini katika akaunti yake hakukuwa na fedha ya kufikia kiasi
hicho.“Nilipomfuatilia alisema atanilipa nisiwe na hofu, lakini cha
kushangaza ni kwamba gari moja Rav 4 ameweka bondi kwa Dk. Mnyau kwa
kipindi kirefu na alishindwa kulikomboa kwa sababu hajalipa fedha,”
alisema Dk. Matech.
Mwandishi wetu alimtafuta Dk. Mnyau
kutaka kujua kama ana gari hilo ambapo alikiri na kusema Nuru
alimkopesha fedha na kuweka gari hilo bondi lakini hajarejesha fedha
hizo hivyo si rahisi kumpa gari.
“Julai 25, mwaka huu, nilimfungulia
kesi namba 8485/2014 yeye na mume wake, Ramadhani katika Mahakama ya
Mwanzo Manzese/Sinza kwa sababu wote nawadai shilingi milioni 12
walizonikopa kwa nyakati tofauti kwa kutegemea gari hili lakini mpaka
sasa hawajalipa,” alisema Dk. Mnyau.
Aliendelea kudai kwamba pamoja
na kupeleka kesi mahakamani, Agosti 5, 13, 19, 29 na Septemba 9, mwaka
huu hawajakanyaga mahakamani, kesi hiyo ipo chini ya Mhe. Zaginga
Patrick.
Mwandishi wa habari hii
aliwatafuta Nuru na mumewe kwa njia ya simu lakini simu zao zilikuwa
zikiita bila kupokelewa na alipowatumia ujumbe kuhusiana na suala hilo
mume wake alijibu hivi:
“Wewe andika unachojua, mimi siwezi kuzungumzia jambo wakati vyombo vya sheria vinashughulikia.”
Post a Comment