Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya
Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha Lami.
Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa
upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete, Mbunge wa
Viti maalum kutoka Chama cha Wananchi CUF, Mbunge wa Simanjiro
Cristopher Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi na
viongozi wengine wa Kitaifa.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara
ya Mayamaya –Mela - Bonga Km 188.15. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni
Mwakilishi wa Serikali ya Japan kushoto, katikati ni Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.
Waziri wa
Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli watano kutoka kulia akicheza
ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Bicha kabla ya uzinduzi rasmi
wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango
cha lami.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli, Mama Salama Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Rehema Nchimbi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi
Gerson Lwenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa
Tanzania Dkt. Tonia Kandiero.
Waziri wa
Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mzee
maarufu wa Wilaya ya Kondoa Balozi mstaafu Mustapha Nyang’anyi kabla ya
uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Kulia ni Naibu
Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
Katapila likisafisha sehemu ya Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Taswira: ‘Mkeka mpya’ Barabara ya Bicha- Kondoa mjini inavyoonekana mara baada ya kukamilika kwake.
Waziri wa
Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Naibu
Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na Mwakilishi Mkazi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia
Kandiero muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya
–Mela-Bonga Km 188.15. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
Post a Comment