SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZA
Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si
lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo
alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa
EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachokukutanisha na watu
mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane
kamili. Mkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama moja ya watu wenye
mafanikio katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ameshawishi vijana
kibao kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka wazi kuwa suala la
lugha ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si jambo la ajabu
sabgabu kuna watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga na lugha ya
kiingereza.
Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini?
RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.
CHUCHU MCHUMBA WANGU
Msanii Vicent Kigosi ambae katika hizi siku za karibuni ilisikika
kuwa yupo katika mahusiano na msanii mwingine wa filamu ambae
anafahamika kama Chuchu Hans hivyo ilipelekea mashabiki wa ukurasa wa
facebook wa EATV kutaka kujua ukweli juu ya mahusiano hayo na kama kweli
jamaa ana mpango wa kumuoa binti huyo au laah, na majibu ya Ray
aliwataka kwamba wawe watulivu muda utakapofika ndio watajua ukweli wote
juu ya suala hilo.
Post a Comment