LICHA ya kutothibitishwa juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa ndoa yake na
mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, mtangazaji maarufu Bongo,
Gardner G. Habash ‘Kepteini’ amenaswa na kabinti akiwa kwenye pozi tata
za kimahaba hivyo baadhi ya watu kuhoji anasaliti ndoa
Tukio
hilo lililojaa viulizo kibao bila majibu, lilifuatiliwa na Oparesheni
Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hatua kwa hatua ambapo lilijiri
Jumatano iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay jijini Dar
kulipokuwa tamasha la wazi la kuibua vipaji vya wasaniii mbalimbali.
Awali,
vijana mbalimbali walipanda katika onesho hilo na kuonesha vipaji
hukubinti huyo jina halikupatikana mara moja, alionekana na rafiki yake
ambapo wote walikuwa ni washiriki katika onesho hilo
Wakati mtangazaji huyo akiwa katika mizunguko yake ufukweni hapo,
ghafla jicho lake lilitua kwa binti huyo na kumfuata kisha kumnong’oneza
kitu (haikujulikana alimwambia nini).
Gardner na mrembo wakiwa pamoja. Huku wapenda ‘ubuyu’ wakimfuatilia
kwa ukaribu, ndani ya muda mfupi, binti huyo alionekana kuelewa
mazungumzo ya Gardner kwa kutingisha kichwa kuashiria ujumbe umemfika
vizuri.
WACHEPUKA
Baada ya Gardner na mrembo huyo kusikilizana, wanahabari wetu
waliwashuhudia wawili hao wakishikana mikono na kuondoka eneo hilo
kwenda kununua vinywaji kisha wakajitenga sehemu wakinywa vinyaji huku
Gadner akiwa amemkubatia kwa nyumba mtoto huyo mzuri na mwembamba kama
Jide.
WAHAMA PAMOJA
Mashushushu wetu waliwashuhudia wawili hao wakipiga misele pamoja
katika maeneo mbalimbali ya ufukwe huo huku mtoto wa kike akiachia
tabasamu zitohuku jamaa akiwa amemzungushia mkono kiunoni, wakizungumza
maneno yalioonesha kuwa wapo kwenye urafiki mzuri.
Akimnong'oneza jambo. WAPENDA UBUYU SASA!
Wakati Gardner akiwa bize akifanya yake huku akiwa ameongeza umakini,
baadhi ya watu ambao ni wepesi kufuatilia mambo ya watu (wapenda
ubuyu/umbeya), walianza kuibua minong’ono kwamba kulikoni mtangazaji
huyo ambaye amekuwa mzito kutamka kwamba hawako pamoja na Jide, ajiachie
kiasi hicho na mrembo huyo.“Jamani huyu si ni Gardner? Vipi tena mbona
anaambatanaambatana na huyu mtoto? Kwa vyovyote ni wazi kabisa kuna kitu
kinaendelea kati yao, maana muda wote wapo beneti.“Duh! Sijui Jide
akiwaona katika pozi kama hizi atajisikiaje kama kweli hawajaachana,”
alisikika mmoja wa wapenda ubuyu.
Baada ya wanahabari wetu kupata walakini na kutaka kuthibitisha hilo,
walianza kumfuatilia hatua kwa hatua mpaka waone mwisho wa mchezo
utakavyokuwa baada ya kuona dalili hizo, kwa kuwa kadiri muda ulivyozidi
kwenda ndivyo mambo yalipozidi kujianika hadharani huku wakijitahidi
kukwepa kamera lakini waligonga mwamba.
WABADILISHANA VINYWAJI
Kuonesha kwamba urafiki wao si wakubahatisha, kuna wakati Gardner na
mrembo huyo walibadilishana vinywaji jambo ambalo lilifanyika chini ya
wapambe wa Gardner ambao walikuwa wakimzingira ili mapaparazi wasiweze
kupata picha kwa urahisi.
Akizidi kuwanaye bega kwa bega. Hata hivyo, mapaparazi wetu
walifanikiwa kuzipata picha hizo kwa kutumia mbinu za kiintelijensia
kama unavyoziona.
WATOWEKA
Wakati mapaparazi wetu wakiendelea kuwafuatilia, ghafla Gardner
alitoweka eneo hilo lililokuwa na watu wengi kisha baada ya muda mfupi
binti naye akatokomea kusikojulikana.
JIDE AAMBIWA AJIONGEZE!
Kwa mujibu wa mashuhuda wa mpango huo, mke wa Gardner, Jide anapaswa
kujiongeza ili kulinda mali yake la sivyo wasichana wa mjini watamzidi
kete.
MSIKIE GARDNER
Alipotafutwa Gander kupitia simu ya mkononi juzi, Alhamisi ili
kuulizwa kuhusu mrembo huyo, mtangazaji huyo alikiri kuwepo Coco kwenye
shoo hiyo lakini hakumbuki ni binti gani amuone vizuri kwenye picha.
“Ebwana ni kweli nilialikwa kwenye hiyo shoo so nilikuwepo lakini kuhusu kabinti siwezi kukumbuka labda nione picha.
“Kweli nilipiga picha na mabinti wengi so sijui ni yupi, unajua
nature (asili) ya kazi yangu (utangazaji) nakutana na watu wengi na
wanapenda kupiga picha na mimi,” alisema Gardner.
Waandishi: Mayasa Mariwata, Denis Mtima na Shani Ramadhani.
Post a Comment