Chama cha Demokrasia na maendeleo
Chadema kimesema kinakamilisha ushahidi ili kwenda mahakamani kupinga
katiba inayopendekezwa kupelekwa katika hatua ya kupigiwa kura ya maoni
kwa madai kuwa katiba hiyo imekosa uhalali kutokana na kukosa theluthi
mbili kutoka upande wa Zanzibar.
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara Profesa Abdalah Safari
ametoa tamkoa hilo wakati akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Iringa na
vitongoji vyake kwenye uwanja wa Mlandege ambapo amebainisha kuwa zoezi
la kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa ndani ya Bunge maalumu la
katiba liligubikwa na mbinu chafu za uchakachuaji wa kura hasa za
wajumbe wa Zanzibar.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Dokta Wilbrod Slaa
amesema chama cha mapinduzi kimeanza kuhujumu mchakato wa uandikishaji
wa wananchi kwenye Daftarai la Makazi kwa kuendesha zoezi hilo kwa siri
huku kikitumia mabalozi wa nyumba kumi wa chama hicho kinyume na
utaratibu wa kawaida ambapo kazi hiyo inapaswa kufanywa na watendaji wa
vijiji kata na mitaa.
Aidha katibu mkuu huyo wa Chadema amewataka wananchi kutodanganyika
na vipengele vya haki za makundi mbalimbali zilizowekwa kwenye katiba
hiyo pendekezwa akieleza kuwa zimewekwa kama chambo kwani haki hizo
zimeondolewa na kifungu cha 21 kinachoeleza kuwa haki hizo hazitadaiwa
mahakamani.
Post a Comment