Kumbukumbu zako ziko sawa kuhusu yale malalamiko ya kukosewa kwa picha ya baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere kwenye noti ya shilingi elfu moja? basi kama hazipo sawa, ichukue hiyo.
Baada ya hayo malalamiko unaambiwa Benki
Kuu ya Tanzania imesema imeanza kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa
kwa picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere
ambapo mkurugenzi wa huduma za kibenki Emmanuel Boaz amesema tayari
benki hiyo imeanza kufanyia kazi hayo malalamiko baada ya kusoma katika
mitandao ya jamii.
Mwananchi wameandika
mkurugenzi huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa mtu
yoyote lakini wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo
“Na sisi tumesoma katika mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo tutachukua hatua za kubadilisha haraka”
“Na sisi tumesoma katika mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo tutachukua hatua za kubadilisha haraka”
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la
picha kukosewa sio geni kwani ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais
wastaafu na BoT ililazimika kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa
Taifa ambapo alitoa mfano wa picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na
kuonekana nguo aliyovaa imefanana na blauzi lakini pia picha ya Rais
Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo
aliwatoa hofu Watanzania kuwa endapo itabainika kama noti hizo zina
kasoro zitarekebishwa ambapo hivi karibuni, mitandao ya kijamii
iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa kwanza wakilalamikia picha hiyo
kwenye noti ya Sh1,000 kukosewa.
Post a Comment