Lango
kuu la kuingia zahanati ya Shirimatunda likiwa na tangazo la kusitishwa
kwa huduma za afya katika zahanati hiyo kwa hofu ya kuwapo kwa mgonjwa
wa Ebola.
Baadhi ya wagonjwa na wauguzi katika zahanati ya Shirimatunda wakihamia
katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Shirimatunda kuendelea na huduma za
tiba ikiwamo utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella
KAZI wa
kata ya Shirimatunda katika maanispaa ya Moshi, wameingiwa na hofu ya
kupoteza maisha yao,kufuatia taarifa za kuwapo kwa mtu anayedhaniwa kuwa
na ugonjwa hatari wa Ebola anayehudumiwa katika zahanati ya kata hiyo.
utokana
na hofu hiyo,halmashauri ya manispaa ya Moshi imelazimika kuifunga kwa
muda usiojulikana zahanati hiyo na kuwahamishia wagonjwa katika
hospitali nyingine ikiwamo ya St Joseph katika manispaa hiyo.
Ripota
wetu ambaye alikuwa eneo la zahanati hiyo alishuhudia baadhi ya
madaktari wakiongozwa na mganga mkuu wa manispaa hiyo,Dk Christopher
Mtamakaya pamoja na wataalamu wengine wa afya wakifanya kikao cha
dharura kujadili hali hiyo.
Kadhalika,waandishi
wa habari waliokuwepo katika zahanati hiyo walishuhudia baadhi ya
wataalamu wa afya wakiwa na mavazi rasmi yanayotumiwa na madaktari
wanaohudumiwa wagonjwa wa Ebola.Pamoja na kikao hicho,Zahanati hiyo
imewekwa tangazo katika lango kuu
linalosomeka 'Huduma zote za afya zimesitishwa kwa muda, Utawala' hali
ambayo imeendelea kuzua maswali mengi kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu katika zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kigongoni,kata ya Shirimatunda ilipo zahanati
hiyo,Juma Sambeke alisema hajashirikishwa katika maamuzi ya kugeuza
Zahanati hiyo kama Karantini ya mtu anayedhaniwa kuwa na Ugonjwa wa
Ebola.
Alisema kuwapo kwa karantini hiyo kumeanza juzi majira ya saa 10 jioni
baada ya kupokea taarifa kutoka afisa mtendaji wa kata hiyo kwamba
zahanati hiyo itafungwa kwa muda ili kumhudumia mtu anayedhaniwa kuwa Ebola.
"Manispaa haikuwa sahihi kuitumia zahanati hii kama karantini ya hofu
ya Ebola, hapa kuna shule ya chekechea, sekondari, seminari ya Don
Bosco na majirani kama unavyowaona....wasipopewa elimu na kama huu ni
ugonjwa wa Ebola watu watakufa sana"alisema.
Sambeke
alisema maeneo yatakayoathirika zaidi na kufungwa kwa zahanati hiyo ni
Shirimgungani,Cherereni ya Moshi vijijini,Karanga, Soweto,Bonite
madukani na mtaa wa Kigongoni ambapo zahanati huudumia zaidi ya watu
5,000 kwa mwezi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Shirimatunda,Felix Mushi alisema
huduma za utoaji wa chanjo ya magonjwa ya Rubella na Surua
zimehamishiwa katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo huku wagonjwa
wengine wakihamishiwa maeneo mengine.
Alisema
tarifa za awali alizopata ni kwamba mtu huyo alipokelewa katika uwanja
wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA), ambapo alisafirishwa hadi
kwenye zahanati hiyo baada ya kudai kuwa na dalilizinazoashiria ugonjwa
wa Ebola.
Aidha
taarifa zaidi zinadai kuwa wataalam wamechukua sampuli kutoka kwa
mgonjwa huyo kwa ajili ya vipimo, ili kujiridhisha, wakati huduma
nyingine za matibabu zikiendelea kutolewa kwa mgonjwa huyo anayedaiwa
kusafiri kutoka nchini Senegal.
Mmoja
wa wakazi anayeishi jirani na zahanati hiyo, Thadei Sangawe,alisema
ameanza kufanya mawasiliano na ndugu wengine waliopo maeneo mengine
mkoani humo ili aweze kuhamisha familia yake kuepuka madhara kama
ugonjwa huo utakuwa wa Ebola.
"Tunaomba viongozi wenye dhamana hususani madaktari watoe taarifa kwa
wananchi juu ya hii hofu iliyopo,maana kukaa kwao kimya kutasababisha
wananchi washindwe kuchukua tahadhari na hivyo kusababisha
madhara"alisema.
Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi wa manispaa
ya Moshi Shaban Mtarambe, alisema hayuko tayari kuzungumza kwa maelezo kuwa suala hilo ni la kitaalam zaidi linalohitaji waataala wa kada ya afya kulizungumzia.
Naye mganga mkuu wa manispaa ya Moshi,Dk Christopher Mtamakaya
alipohojiwa kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa mgonjwa huyo hakuwa
tayari kuzungumza zaidi na alipotumiwa ujumbe wa simu ya mkononi
alijibu kwa kifupi, huo ni Uvumi.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa mkoa huo,Dk Mtumwa Mwako alipohojiwa
kuhusiana na kuwapo kwa mgonjwa huyo naye alisema hafahamu na aliomba kupewa
muda kwani alikuwa katika kikao.Kuhusiana na suala la mgonjwa
huyo,katibu tawala wa mkoa huo, DkFaisal Isa alisema taarifa za kwanza
anapata kutoka kwa mwandishi wetu na akaomba muda wa kufuatilia zaidi.
Post a Comment