Ama kwa hakika duniani kuna mambo!
wachuuzi wa kahawa yenye vijimambo ndani yake,ambayo ukiinywa tu basi
inakupa mzuka wa kufanya ngono kwa kiwango cha hali ya juu na biashara
inawaendea vyema katika mitaa ya Harare nchini Zimbabwe.
Kahawa
hiyo huuzwa kati ya dola za kimarekani 3 hadi 5 kwa kifuko kidogo
kinachotosha kikombe kimoja cha chai, na bei hiyo itategemea jinsi wewe
ulivyo mtaalamu wa kuomba punguzo la bei inaweza kushuka.
Wachuuzi
hao wa mitaa ya Harare wamezungumza na kudai kuwa kahawa hiyo
huwasaidia wanaume kupata hamu ya kufanya ngono kwa muda mrefu
Zaidi,lakini pia humchelewesha mwanaume kupata mshindo kwa muujibu wa
utafiti wao.
Pindi tu uinunuapo kahawa hiyo,wachuuzi hao hukupa
maelekezo kuwa uinywe dakika 15 kabla ya tukio lenyewe na humpa nguvu
mtumiaji ya kufanya ngono kwa saa sabini na mbili,ingawa madai hayo
hayajathibitishwa kitabibu.
Wachuuzi hao wameamua kufanya biashara yao katika mtindo wa aina
yake,kwa kuiuza kahawa hiyo katika maeneo maarufu nchini Zimbabwe yenye
mikusanyiko ya watu kama eneo la KwaMereki kwenye viunga vya bustani ya
kitongoji cha Warren, Zindoga eneo lililoko kwenye maporomoko ya maji
(Waterfalls) na eneo la vilima la KuHuku .
Kitu cha kuvutia
biashara hiyo hufanywa na wachuuzi wa kike wafanyao kazi katika duka
kubwa la Fife Avenue Shopping centre wenye kutoa ushuhuda na kukubali
kuwa waume zao waliitumia kahawa hiyo na wakayaona matokeo yake nao
wakafaidi kwani uwezo wao uliongezeka maradufu.
Ingawa wanawake
hao pamoja na kukubali na kutoa ushuhuda huo, bado hawako tayari
kuelezea wapi wanakozinunua kahawa hizo za majamboz na kwa sasa mjini
Harare mahitaji ya kahawa hiyo ni makubwa mno na ni rahisi kuitumia
kwani unaweza kuitumia kwa maji moto ama baridi anaeleza muuzaji
aliyejitaja kwa jina moja la Anna.
Anna anasema wateja wake
wakubwa ni waume kwa wake ingawa wanawake wana aibu kuinunua kahawa hiyo
hadharani kuliko wanaume wao hawana aibu pindi wanapotaka kahawa hiyo
kwa matokeo mazuri ya kulinda heshima shughulini.
Kwa muujibu wa
daktari mmoja nchini Zimbabwe aliyekataa kutajwa jina lake amesema
kwamba tatizo la nguvu za kiume nchini Zimbabwe ni kubwa mno kwa wanaume
walio wengi na linakua siku hadi siku na kusema ni tatizo kubwa.
CHANZO:BBC
CHANZO:BBC
Post a Comment