Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata mlo nyumbani kwa Balozi Lucas
Mtumbuka (kushoto)wa Shina namba moja eneo la Mkimbizi, alipokwenda
kumtembelea yeye na wananchama wake wakati wa ziara ya kuimarisha uhai
wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Jimbo la
Iringa Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO
BLOG
Kinana akichukua mhogo ambao ni sehemu ya vyakula alivyoandaliwa na balozi
Watoto wakipanda kwenye uzio wa nyumba ili wapate kumuona Kinana alipomtembelea Balozi, Lucas Mtumbuka, eneo la Mkimbizi
Kinana
akiingia kwenye ukumbi kuzungumza na wanachama 707 wa kikundi cha
Iringa Masoko Vicoba ambapo aliahidi kuwasaidia kuipata mkopo mkubwa wa
fedha watakazokuwa wanakopeshana.
Kinana
akizungumza na madereva wa daladala baada ya kuzindua tawi la
wakareketwa wa CCM, mjini Iringa leo. Tawi hilo lina wanachama 60.
Mama
Lishe akimnawisha mikono Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambapo
yeye na viongozi pamoja na baadhi ya wananchama wa CCM walikwenda kupata
chakula cha mchana kwa mama lishe katika Soko Kuu la Iringa leo.
Kinana
akiapata mlo wa mchana kwa mama lishe mjini Iringa leo wakati wa
mapumziko ya ziara ya kuimarisha uhai wa chama.Kulia ni Mwenyekiti wa
CCM WIlaya ya Iringa Mjini, na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu.
Mbunge
wa Viti Maalum, Rita Kabati (kushoto) akiwa na viongozi wengine wa CCM
wakipata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, mjini Iringa leo.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga (katikati) akiwa na viongozi
wengine wa CCM wakati wa chakula cha mchana kwa mama lishe.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chongolo, akipata mlo huo wa mchana kwa mama lishe.
Wanahabari ambao baadhi yao wako kwenye msafara wa Kinana wakipata mlo wa mchana kwa mama lishe
Kinana
akiondoka baada ya kupata mlo wa mchana kwa Mama Lishe, katika Soko la
Iringa Mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihuubia huku mkono wake
ukiwa umefungwa POP, katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya
Mwembetogwa, mjini Iringa leo wa kuhitimisha ziara ya siku sita mkoani
Iringa ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia
ufumbuzi.
Wananchi wakicheza kwa furaha wakati kikundi cha Bendi ya CCM, kikitumbuiza kwa wimbo wa Ilani ya Chama wakati wa mkutano huo.
kikundi cha Bendi ya CCM, kikitumbuiza kwa wimbo wa Ilani ya Chama wakati wa mkutano huo.
Ni furaha kwa kwenda mbele kadri muziki wa wimbo huo ulipokuwa unapigwa uwanjani hapo
Nape akifarijiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo wakati wa mkutano huo
Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, akihutubia katika mkutano wa
hadhara na kuelezea mipango ya chama hicho kulikomboa jimbo la Iringa
linaongozwa sasa na Chadema.
Nape akishuka jukwaani baada ya kuhutubia katika viwanja vya Mwembetogwa, Iringa Mjini
Aliyewahi
kuwa mgombea ubunge Jimbo la Kalenga wa Chadema kura za maoni, Sanga
Abubakar akitangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano
huo.
Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Mdillah Sekomu akitangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM
Msemaji
wa Bodaboda, Adam Kindole Mkoa wa Iringa, akielezea jinsi
wanavyonufaika na CCM kwa biashara yao ya kubeba abiria mjini
Waendesha Bodaboda wakishangilia risala iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho cha waendesha pikipiki
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia katika mkutano huo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha CCM, Daniel Chngolo akimuaga Kinana Uwanja wa Nduli akirejea Dar es Salaam.
Kinana akiagana na viongozi wa CCM uwanjani hapo
Kinan akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiingia kwenye ndege, tayari kwenda Arusha na hatimaye DSM
Kinana akiagana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu
Ndege iliyombeba katibu mkuu
Viongozi wa chama na Serikali wakipungia mkono wakati ndege iliyombeba Kinana ikipaa
Post a Comment