Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa Kilolo
Mnadani waliojitokeza kumlaki katika ziara yake wilayani Kilolo Kinana
yuko mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita ya kikazi akiongozana na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi, Ziara hiyo ina lengo la
kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2014 na
kuhimiza uhai wa Chama.
MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa Peter Msolla akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua
matofali ya kikundi cha vijana cha Muungano ambacho kina jumla ya vijana
arobaini waliopata mafunzo ya kufyatua matofali na ujenzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wajumbe wa
halmashauri kuu ya wilaya ya Kilolo katika ukumbi wa halmashauri ya
wilaya ya Kilolo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha
Utengule kata ya Ihimbo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa uchaguzi wa
Serikali za mitaa mwezi Desemba CCM itashinda kwa kishindo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha
utengule kata ya Ihimbo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo
aliwaambia viongozi wa Kata na Vijiji pamoja na ngazi ya wilaya wafanye
mikutano na wananchi wao na waruhusu maswali ilikujua changamoto
zinazowakabili wananchi .
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Utengule Ndugu Pancras Mkakatu ambaye ni mwanachama wa
Chadema akiongea na wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ambapo alimpongeza sana Katibu Mkuu wa CCm kwa kazi
nzuri anayofanya na kueleza kuwa yeye ni CCM ila alitoka tu kwa sababu
ya migongano na viongozi wengine wa CCM .
Zahanati ya Kijiji cha Utengule ambayo imekamilika ilabado haijapata madaktari
Mwenyekiti
wa Kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Uwindi Ndugu Charles
Kigwile akiuliza swali linalohusu ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ambao
umesimama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhiwa mkuki kama ishallah ya kuwa Mtemi wa Wahehe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwashukuru wananchi wa kijiji
cha Utengule kwa kumpa heshima ya kuwa Mtemi kwenye kijiji chao
Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na Watemi wenzake wa kijiji cha Utengule.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaaga wananchi waliofurika kwa wingi kwenye mkutano wake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mikono ya kwa heri na wananchi wa kijiji cha Utengule.
Madarasa ya shule ya msingi Iwindi wilayani Kilolo mkoani Iringa
Mwalimu
Josephine Konga wa Shule ya msingi akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana uchache wa vyumba vya madarasa katika shule
hiyo kiasi kupata shida sana katika kufundisha.
Post a Comment